NA; HERI SHAABAN
DIWANI wa Kata ya Ilala Saady Khimji amesema Mradi wa kuboresha Miundombinu awamu ya pili DMDP unaotarajia kuwa mkombozi wa kujenga Barabara za Kata ya Ilala kiwango Cha lami
Diwani Khimji ambaye ndio NAIBU MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam aliyasema hayo katika kikao cha Wananchi Pamoja na kusikiliza kero za Wananchi kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa Serikali za mitaa Karume Haji Bechina
Diwani Khimji alisema Kata yake ya Ilala ina changamoto kubwa ya Barabara na Miundombinu kwa ujumla , Barabara zote zipo chini ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA lakini changamoto iliyopo TARURA aina pesa inategemea pesa kutoka Serikali.
“Mkakati wangu katika kata ya Ilala itakuwa mkombozi wa Barabara za mitaa Mradi wa Kuboresha Miundombinu DMDP awamu ya pili kujenga Barabara za Kata yetu hivyo Wananchi mvute subira tusubiri Utekelezaji wa miradi mikubwa”alisema Khimji.
Diwani Khimji alisema Barabara KM 14 za Ilala zote zitawekwa lami Mji wa Ilala itapendeza na kuwa wa kisasa.
Wakati huo huo Diwani Khimji alipokea changamoto za kero kuhusiana na Gereji Bubu Ilala alisema kuna vijana 300 washakuwa Jamii ya Watu wa Ilala wamekulia eneo hilo na wengine wameoa wanajishughulisha na masuala ya Gereji
Pia alizungumzia kero ya Magari kudaiwa ushuru majumbani wa Paking na TARURA alisema alishafikisha katika vikao vya Halmashauri ya Jiji na Madiwani wa Ilala wameshaweka mikakati yao na mazimio hivyo Wananchi aliwataka wavute subira kitendo Cha kudaiwa ushuru majumbani mwao wa magari
Wakati huohuo Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady Khimji alikabidhi Sadaka ya FUTARI kwa waumini wa Dini ya Kislaam futari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Karume Haji Bechina kwa ajili ya wananchi wake.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti BECHINA alisema Kikao hicho kilikuwa kinajadili KERO za Wananchi , masuala ya Ulinzi Shirikishi,pamoja na utoaji elimu ya SENSA ya makazi kwa Wananchi wa Ilala.
BECHINA alisema zoezi la anuani za makazi Mtaa wa Karume wamefanya vizuri na linaendelea katika mtaa huo. Changamoto amna
Kwa upande wake OCD KARIAKOO William Solla alisema Kata ya Jangwani na Ilala Vijana wengi wanaongoza kwa Dawa za Kulevya wamekuwa mateja pia kuna nyumba za Biashara za Gongo zinachangia kuharibu makundi ya vijana .
Kamanda William alisema mikakati ya Jeshi la Polisi kuhusu Kata ya Ilala na Jangwani Jeshi la Polisi limejipanga kufanya Oparesheni maeneo hayo nyumba kwa nyumba .
Aidha Kamanda William aliwataka Wenyeviti wa SERIKALI za Mtaa kuimalisha Ulinzi Shirikishi Katika maeneo yao ikiwemo kutambua wageni wanaoingia na wanaotoka
Mwisho.