Baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristo wakishiriki kupata futari hiyo na wenzao wa Kiislam.
atibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam (BAKWATA) Sheikh Burhan Mlau akizungumza kwenye futari hiyo lliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu iliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi jana.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akiwapa tende wanafunzi waliohudhuria futari aliyoiandaa iliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ikungi jana.
Watoto wakipata futari
Wageni waalikwa wakipata uji kabla ya kupatiwa futari.
Mke wa Mchungaji Samuel wa Kanisa la FPCT, Ikungi akishiriki kuwagawia watoto tende wakati wa hafla hiyo. Jambo ili linaonesha mshikamano mkubwa baina ya Waislam na Wakristo hongera sana Mbunge Mtaturu
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa (kushoto) na Miraji Mtaturu (kulia) wakiwa wamempokea Alhajj Sheikh Salum Mubaraak Mtimkavu kutoka Arusha ambaye alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Mbunge Mtaturu akizungumza kwenye hafla hiyo wakati akishukuru kufika kwa wageni waalikwa.
Na: Dotto Mwaibale, Singida
WAISLAM na Wakristo wametakiwa kuendelea kudumisha upendo na Amani walionao jambo ambalo linampendeza Mwenyezi Mungu. Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam
(BAKWATA) Sheikh Burhan Mlau wakati akizungumza kwenye futari lliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu iliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ikungi jana.
(BAKWATA) Sheikh Burhan Mlau wakati akizungumza kwenye futari lliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu iliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ikungi jana.
“Ndugu zangu nawaombeni tuendelee kudumisha upendo uliopo baina yetu Waislam na Wakristo ambao upo enzi na enzi kwani kuna wenzetu katika nchi nyingine wameingia katika mapigano kwa sababu ya imani za kidini lakini sisi mambo haya hayapo kabisa” alisema Mlau
Mlau alimpongeza Mtaturu kwa kuandaa hafla hiyo na kuwaalika viongozi mbalimbali wa kikristo jambo ambalo limekuwa likifanyika na wakristo kuwaalika Waislam wanapokuwa na hafla kama hiyo ambapo alimshukuru pamoja na familia yake kwa jambo hilo..
Akitolea mfano wa upendo uliopo baina yao alisema Chamwino Dodoma kuna msikiti mkubwa na nyumba ya Mufti imejengwa kwa michango ya wakristo kwa uhamasishaji uliofanywa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli na kuwa jambo hilo ni la kujivunia watanzania.
Halikadharika Mlau alisema ataunda kamati itakayo wahusisha viongozi wazawa ili kusimamia mapato yatokanayo na vibanda vya biashara vilivyopo katika msikiti wa wilaya hiyo ambayo yamekuwa ni chanzo kikubwa cha kugombana
Akiongelea kuhusu mahusiano baina ya Waislam na Wakristo Alhajj Sheikh Mubaraak Mtimkavu kutoka aliyekuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye hafla hiyo aliyaomba makundi hayo kujiepusha na mifarakano na kumaliza changamoto zao kwa usiri bila ya kutoa nje jambo litakalo waongezea heshima na kueleza kuwa Mungu ndivyo anavyopenda.
Sheikh Mtimkavu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Twariga Qadiriya Arraziqiya alipata fursa ya kuwaombea dua wageni wote waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo muhimu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akizungumza kwenye hafla hiyo alionesha kukerwa kwa migogoro baina ya waislam kwa waislam ya kugombea misikiti kwa lengo la kujinufaisha na kuwa hali hiyo inaufifisha uislam na aliomba jambo hilo la aibu likomeshwe.
Aidha Likapakapa alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge Mtaturu kwa kuandaa futari hiyo na kusema kuwa jambo hilo alilolifanya kwa wananchi wa wilaya hiyo ni jambo jema machoni kwa Mungu.
“Mtaturu wala sio tajiri lakini ameona ni vizuri kuandaa futari hii kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Ikungi hivyo tunamuombea kwa Mungu ampe maisha marefu na kumzidishia kile alichokitoa” alisema Likapakapa.
Mtaturu aliwashukuru watu wote waliokuwepo kwenye hafla hiyo kwa kufika kwao na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakapo wadia ili Serikali ipate idadi kamili ya watu na kuweza kupanga vizuri mipango yake ya maendeleo
Baadhi ya wageni waalikwa walioalikwa kwenye hafla hiyo Yatima, wajane, wahitaji, viongozi mbalimbali wa chama na Serikali wa wilaya hiyo