Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer (katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa TEF Bakari Machumu (kulia) mara baada ya Balozi huyo alipowasili kufungua Semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwaajili ya kuwajengea uwezo waandshi hao juu ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya vyombo habari chini kilichofanyika leo Oktoba 20,2022 katika Hoteli ya Slipway Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile akizungumza alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi katika Semina hiyo ilichofanyika leo Oktoba 20,2022 Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer akizungumza wakati alipokuwa akifungua rasmi Semina hiyo iliyowakutanisha wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kujadili mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya habari Jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Kikao hicho ambao ni wahariri na waandishi wa habari waliofika kuhudhuria kikao hicho.
Mhariri wahabari wa Clouds TV na Clouds FM Joyce Shembe (kulia) akiwa na Mhariri wa habari wa BBC Swahili wakifuatilia hotuba ya Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer katika kikao hicho.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Anitha Mendoza (kushoto) akiwa na Ofisa kutoka katika Taasisi hiyo Elizabeth Chanzi katika kikao hicho.
Mwenyekiti Mstaafu wa TEF Theophil Makunga akizungumza katika kikao hicho alipokuwa akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kufungua kikao hicho Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa TEF Bakari Machumu (kushoto) katika mkutano huo.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAM.
Waandishi wa habari nchini wameshauriwa kuandika habari zinazotetea taaluma yao na maslahi yao kwa ujumla.
Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 20,2022 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na jukwaa hilo kwa lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu utetezi wa mabadilko ya Sheria ya vyombo vya habari.
Balile amesema kuwa waandishi wa habari wana jukumu kubwa la kutetea taaluma yao na maslahi yao kwa ujumla lakini zipo baadhi ya sheria zinasababisha kushidwa kufanya kazi zao kwa weledi na hivyo kushidwa kutetea haki na maslahi yao.
“Kuna baadhi ya taasisi zinasema wanatetea haki za waandishi lakini wao sio waandishi na hawazijui changamoto za waandishi ndio maana tukasema tuanze kutetea haki na maslahi yetu wenyewe,” amesema Balile.
Aidha Balile amezungumzia vifungu vya sheria ya habari na kueleza wapo kwenye mchakato wa kuona namna ambavyo Bunge litapitia upya sheria hizo hususani ni zile zinazoleta vikwazo kwa waandishi wa habari ili vifanyiwe marekebisho.
Kwa upande wake Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt. Wiebe de Boer akizungumza alipokuwa akifungua semina hiyo amelipongeza Jukwaa la Wahariri (TEF) kwa kuwa na programu za kuwajengea uwezo wanahabari ili wafanye kazi kwa weledi na kwamba ubalozi huo uko tayari kushirikiana jukwaa hilo.Â
PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Dkt.Wiebe de Boer (kulia) akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (kushoto) mara baada ya kufungua rasmi kikao hicho.
PICHA ZA BALOZI WA UHOLANZI AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA TEF.