Benki ya Absa Tanzania imesema itaendelea kudhamini mbio zaidi nchini ili kudumisha utamaduni wa afya njema huku ikipamba mbio za Dar City Marathon iliyofanyika Jumapili Jijini Dar es Salaam
Akizungumza baada yam bio hizo, Mkuu wa Masoko na Uhusiano Aron Luhanga alisema Absa imerishishwa na na namna mbio hiyo iliendeshwa na benki hiyo ilikuwa na washiriki 45 kwa ujumla katika mbio za km 5, km 10 na km 21.
“Kwetu sisi tunaamini katika wafanyakazi kuwa na afya ya mwili lakini pia afya ya akili ili waweze kufanya kazi vizuri ndio maana tunajitahidi kushiriki katika mbio nyingi,” alisema.
Bw. Luhanga alisisitiza kuwa mwakani pia watadhamini mbio hiyo huku wakitarajia kuwa itawavutia wau wengi zaidi. “Hiini mara ya pili wanafanya mbio hii na kwa kweli muitikioni mzuri sana na kuna dalili kuwa kwa miaka ijayo mbio hii itakuwa kwa kasi sana.”
“Tunaungana na waandaaji katika kukuza utamaduni wa kuzingatia afya njema na pia kulitangaza Jiji la Dar es Salaam duniani,” alisema.
Alisema mbio hiyo pia ilitoa fursa nzuri kwa wafanyakazi wa Absa na wateja kujumuika na wadau wengine kutoka mashirika mengine na kubadilishana mawazo huku wakifurahia burudani katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
“Kama unavyoona katika banda letu wafanyakazi wamechangamka lakini pia tuna wateja wetu ambao wamejumuika na sisi katika mbio hii,” alisema.
Pamoja na kukimbia wafanyakazi wa Absa na wateja pia walipata fursa ya kupima afya zao ikiwemo presha, uzito kabla na baada yam bio na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu waliokuwa katika banda la Absa.
MWISHO