Home BUSINESS WAZIRI KIJAJI AIPONGEZA STAMICO KUZALISHA MKAA MBADALA ‘RAFIKI BRIQUETTES’

WAZIRI KIJAJI AIPONGEZA STAMICO KUZALISHA MKAA MBADALA ‘RAFIKI BRIQUETTES’

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Ashatu Kijaji amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuzalisha mkaa mbadala ambao ni suluhisho katika utunzaji wa mazingira.

Akiwa katika banda la STAMICO wakati wa maonesho ya teknolojia ya Madini Mhe. Kijaji amesema STAMICO imeleta bidhaa mpya ambayo ni mkombozi kwa wananchi na kulishukuru Shirika hilo kwa kuanza uzalishaji wa mkaa huo ili kuhakikisha biadhaa hiyo inapatikana kila mahali hapa nchini.

Amesema ni wakati sasa wa kuangalia namna nzuri ya kuisambaza teknolojia hio kwa watu wengine ili kuongeza wigo na kasi ya uzalishaji.

“STAMICO mnatakiwa kusambaza teknolojia hii kwa watu wengine zaidi ili waweze kutengeneza mkaa na kuusambaza kwenye maeneo yao na kwa kufanya hivyo mtaongeza ajira kwa Watanzania” Mhe Kijaji alisisitiza.

Akielezea teknolojia ya kutengeneza mkaa huo Meneja Masoko na Uhusiano Bw. Geofrey Meena amesema STAMICO imetumia teknolojia ya kisasa ili kufanya mkaa huu uwe rafiki kwa matumizi yake.

“Kwa sasa STAMICO imejizatiti kuongeza uzalishaji kwa kuleta mitambo mikumbwa yenye uwezo wa kuzalisha tani 20, na kwa kuanzia itawekwa katika mikoa ya Pwani na Songwe jambo litakalosaidia kuongeza wigo wa matumizi wa mkaa huu”

Maonesho haya yamefungwa rasmi leo tarehe 8 Septemba 2022.

Previous articleKAMPENI YA JIFICHUE YAZINDULIWA KWAAJILI YA KUTOA ELIMU YA AFYA YA AKILI
Next articleMCHANGO WA SEKTA YA MADINI WAZIDI KUIMARIKA: DKT. KIJAJI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here