Na: Mwandishi Wetu
KIKOSI Cha Yanga leo kinashuka dimbani kuchuana na Al Hilal ya Sudan katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe amesema kuwa kikosi kimejipanga vyema kuelekea mchezo huo.
Ameongeza kuwa kikosi hakitakuwa tayari kurudia makosa yaliyofanyika katika msimu uliopita kwa kutolewa kwenye michunano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Rivers United.
Amefafanua kuwa kwa sasa wanatambua mashabiki wanahitaji matokeo hata wachezaji nao wanatambua kinachohitajika ni ushindi.
“Wachezaji wamejipanga vyema kuelekea mchezo huo pamoja na benchi la ufundi, viongozi tupo vyema na tunachosubiri ni kupambana na kupata matokeo nyumbani,” amesema.
Ameongeza kuwa wanajua hitaji la mashabiki wanahitaji ushindi, hivyo amewataka wadau na mashabiki kujitokeza kuwa wingi katika uwanja ili kuongeza hamasa kwa wachezaji pindi wakiwa uwanjani.