Home LOCAL WATAALAM WA MAABARA WAASWA KUBORESHA UBORA WA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA

WATAALAM WA MAABARA WAASWA KUBORESHA UBORA WA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA

   Na: Englibert Kayombo – WAF, Dar Es Salaam.
 
Serikali imewataka wanataaluma ya maabara kuboresha ubora wa huduma za maabara ili kuwezesha upatikanaji wa matokeo sahihi ya uchunguzi wa magonjwa yatakayowezesha wananchi kujua afya zao pamoja na kupata matibabu sahihi.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel leo alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwenye ufunguzi wa Kongamano la 35 la Kisayansi la Wataalam wa Maabara lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar Es Salaam.
 
Dkt. Mollel amesema kipaumbele cha Sekta ya Afya kwa sasa ni ubora wa huduma hivyo kuwasisitiza wataalam hao kufanya kazi kwa ufanisi na kuboresha huduma wanazotoa kwa wananchi.
 
“Watu wa maabara mkikosea matokeo yake yanaonekana mara moja na wakati mwingine yanagharimu maisha ya watu, Waziri Mkuu amewaomba mkifika kwenye maeneo yenu ya kazi mkasimamie ubora wa huduma kwa sababu maisha yetu yapo mikononi kwenu” amesema Dkt. Mollel
 
Dkt. Mollel amesema Wanataaluma wa Maabara ni kiungo muhimu katika upatikanaji wa matibabu sahihi kwa mgonjwa hivyo Serikali inatambua na kuthamini mchango wao katika kuboresha huduma bora za afya nchini.
 
“Tumepitia vipindi vya milipuko tofauti ya magonjwa ikiwemo, UVIKO-19, Homa ya mgunda na sasa Ugonjwa wa Ebola nyie mmekuwa msingi wa kutuvusha na kutuweka sisi salama” amesema Dkt. Mollel
 
“Maabara ni moyo wa Hospitali, Hospitali zetu zinetegemea ufanisi wa Idara hii kwa ajili ya usalama wa afya zetu, tunawashukuru sana” amesema Naibu Waziri Dkt. Mollel.
 
Aidh Dkt. Mollel amesema kuwa Serikali imepokea changamoto iliyowasilishwa ya masuala ya kimuundo wa utumishi wa kada ya wataaluma wa maabara na kuahidi kuwa maoni ya wadau hao yamepokelewa na Serikali itayafanyia kazi ili kuwa na muundo wenye tija na kuinua taaluma hiyo.

Mwisho.

Previous articleWAKALA WA VIPIMO (WMA) YATOA ELIMU KWA WANANCHI NA WADAU WA SEKTA YA MADINI GEITA
Next articleSHINYANGA WAKAA MGUU SAWA KUPAMBANA NA EBOLA… RC MJEMA AAGIZA WATENDAJI WOTE KUFANYIA KAZI HARAKA MAAGIZO YOTE YANAYOTOLEWA NA RAIS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here