Home BUSINESS WAZIRI JAFFO ATEMBELEA BANDA LA PSSSF MAONESHO YA SEKTA YA MADINI GEITA

WAZIRI JAFFO ATEMBELEA BANDA LA PSSSF MAONESHO YA SEKTA YA MADINI GEITA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) akizungumza  na Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya tano ya Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili EPZA Geita.

Waziri Jaffo amekuwa mgeni rasmi wa siku ya leo Oktoba 6,2022 ambapo ameiagiza PSSSF kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka (Dustbins) katika maeneo mbalimbali nchini kwa namna ambavyo PSSSF watapendekeza ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 ya Rais Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa Mazingira.

Aidha Waziri Jaffo ameipongeza PSSSF kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulipa mafao kwa wakati na kuwawezesha wastaafu kuwa na uhakika wa maisha yao baada ya kustaafu.

(Picha Na: Hughes Dugilo)

Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) alipofika kwenye Banda la Mfuko huo  kujionea shughuli wanazozifanya katika Maonesho ya Madini Geita.

Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko huo katika Banda lao.

Previous articleWAZIRI JAFFO AIPONGEZA BUCKREEF KUPANDA MITI KATIKA VIJIJI VINAVYOZUNGUUKA MGODI HUO
Next articleTANZANIA, INDIA KUIMARISHA SEKTA YA UCHUMI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here