*Serikali yajipanga kuyapandisha hadhi Maonesho ya Madini Geita kuwa ya Kimataifa*
Na: Costantine James -GEITA.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Ally Gugu amesema Serikali ina mpango wa kuyapandisha hadhi maonesho ya kitaifa ya teknolojia ya madni yanayofanyika mkoani Geita kuwa ya kimataifa lengo likiwa ni kupanua wigo kwa wadau mbalimbali wa sekita ya madini pamoja na wajasiliamali kupata uzoefu kutoka katika kimataifa ya kigeni.
Ameyasema hayo leo Octoba 4,2022 katika viwanja vya EPZA Bombambili Mkoani Geita alipotembelea mabanda mbalimbali ya Wajasiriamali na Sekta za Umma katika maonesho ya 5 ya kitaifa ya teknolojia ya madini nakujionea jinsi washiriki wa maonesho hayo walivyotumia fursa hiyo kuonesha bidhaa zao pamoja na bunifua mbalimbali katika sekta ya madini.
Amesema kutokana na mwitikio mkubwa wa washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ipo haja ya kuyapandisha maonesho hayo nakuwa maonesho ya kimataifa ili kushirikisha nchi mbalimbali zitakazowawezesha wajasiriamali nchini na wadau katika sekita ya madini kuweza kuonesha bidhaa zao pamoja na kupata masoko ya kimataifa.
Amesema maonesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini yakipewa hadhi yakuwa maonesho ya kimataifa yatawasaidia wajasiriamali pamoja na wadu katika sekita ya madini yakuweza kutoka na kuuza huduma zao na bidhaa nje ya nichi.
Maonesho haya yanawawezesha wajasiriamali kukuza kipato chao pamoja na kupata fursa ya kukutana na taasisi mbalimbali za kibenki zitakazo wasaidia kwa kuwakopesha ili kuwawezesha kuongeza mitaji yao.
Amewataka wchimbaji wadogo wa madini kutumia vema fursa ya uwepo wa maonesho hayo katika kujifunza teknolojia mpya za uchimbaji wa madini pamoja na uongezi wa thamani kwenye madini ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji katika shughuli zao.