Home LOCAL WILAYA YA IKUNGI, KIWOHEDE KUANZA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MILIONI...

WILAYA YA IKUNGI, KIWOHEDE KUANZA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MILIONI 117

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro akionesha picha inayoonesha jinsi jengo la kisasa la MKONO SHUFAA lenye thamani ya Sh.117 Milioni litakalo jengwa na Shirika lisilo la Kiserikali la KIWOHEDE wilayani humo baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo hilo, Justa Mwaituka (kulia) ambae kwa pamoja wamekubaliana kuanza ujenzi huo wakati wowote kuanzia sasa.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro akiangalia nyaraka zinazoonyesha ujenzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la KIWOHEDE, Justa Mwaituka. 

Na: Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Ikungi, Jerry  Muro amehitimisha mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la KIWOHEDE Mama Justa Mwaituka ambae kwa pamoja wamekubaliana kuanza ujenzi wa jengo la kisasa la MKONO SHUFAA lenye thamani ya Sh.117 Milioni. 

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Muro alisema  jengo hilo litajengwa wakati wowote kuanzia sasa katika Hospitali ya Wilaya ya Ikung kwa ajili ya kuratibu na kusimamia shughuli za upingaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike na kiume na wanawake katika Wilaya ya Ikungi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wilaya zinakomesha matukio na vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa watoto na wanawake. 

DC Muro alisema wao kama wiliaya wameona waweke utaratibu utakaotuwezesha kupambana na matukio yanayozidi kuongezeka ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto wetu na wanawake kwa kujenga mifumo imara ya kuratibu na kushughulikia changamoto hii ambayo imeendelea kuongezeka katika wilaya. 

Muro aliongeza kuwa maono ya wilaya ni kuona wanabadili mwelekeo ambao hautamtazama mtoto wa kike peke yake bali utawatazama watoto wote kama wahanga wakuu wa matukio ya ubakwaji, ulawiti, utumikishwaji wa kazi za majumbani na vitendo vingine vya ukatili ikiwemo watoto wanaozunguka na kuombaomba mitaani. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa KIWOHEDE Mama Mwaituka alisema wameridhishwa na jinsi wilaya inavyopambana katika kukomesha vitendo vya ukatili wa kijinsi na kwa kipindi chote walichofanya kazi Ikungi wameridhishwa na ushirikiano na namna halmashauri inavyotekeleza maelekezo ya kutokomeza vitendo hivyo japo bado jitihada zaidi zinahitajika katika kumaliza changamoto hiyo. 

DC Muro alitumia nafasi hiyo kulishukuru shirika hilo kwa kuendelea kufanya kazi na wilaya hiyo hasa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Timu yake kwa kuratibu jambo hilo kwa haraka na sasa wanakwenda kuongeza thamani katika kuwalinda watoto na wanawake katika Wilaya kwa mkakati na ubunifu mpya.

Previous articleWAZAZI MKOANI RUVUMA WAHIMIZWA KUWAUNGANISHA WATOTO WALIOPO SHULENI NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA
Next articleTAKUKURU SINGIDA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO YA ZAIDI YA SH. BILIONI 4.4
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here