Na: Heri Shaaban (Ilala ).
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam AMOS MAKALA ameagiza kila halmashauri katika mkoa huo wawe na Dampo lao la kutupa taka .
Mkuu wa Mkoa Amos Makala ,ameyasema hayo Wilayani Ilala Viwanja yya Mnazi Mmoja wakati wa siku ya usafi na uzinduzi magari ya kisasa ya kuifadhia taka ambayo yanauwezo wa kubeba taka tani 26.
“Serikali ina mikakati ya kuboresha Dampo nagiza kuanzia sasa kila Halmashauri ifanye mpango iwe na Dampo lao isitegemee Dampo la Pugu Nyamwezi kutupa taka zao” alisema Makala
Alisema kila Halmashauri wakiwa na sehemu ya kutupa takataka Wakandarasi wa usafi wataweza kusafirisha taka kwa wakati mji wa Dar es Salaam utavutia kwa usafi .
Amepongeza KAMPUNI ya Kajenjele kwa magari ya kisasa ya usafi magari Bora wamejipanga vizuri katika uwekezaji Dar es Salaam na Morogoro ina fanya vizuri ameagiza KAMPUNI nyingine kuiga mfano huo wa Kajenjele
Makala ameagiza Dar es Salaam katika kulipendezesha Jiji hilo Majukumu ya usafi wapewe Wakandarasi wenye uwezo na vifaa vya usafi wasigawe tenda za usafi kwa kujuana
Aidha alipongeza Kampuni ya Kajenjele inayofanya Shughuli za usafi Dar Salaam na Morogoro imekuwa ikisaidia Serikali katika kulipendezesha Jiji hilo imekuwa ikijitolea kufanya usafi maeneo mbalimbali ya Kampeni ametaka Wakandarasi wengine kuiga .
Wakati huo huo alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuna watu Wana haribu Bustani Kisutu amewataka Maafisa watendaji Kata kufatilia hilo kuwachukulia hatua Ili wasiharibu Jiji letu ambalo linavutia kwa Sasa.
Katika hatua nyingine alisema Serikali inatarajia kufunga Kamera za kisasa kuanzia uwanja NDEGE wa Mwalimu Julius Nyerere mtu akifanya jambo lake Serikali itamuona na kumchukulia hatua
Mwisho