Na: Mwl Udadis, Sumbawanga
Historia inaonyesha kuwa orodha ya viongozi mashuhuri Duniani imejawa na watu wanaopenda kufanya mageuzi chanya yenye kuleta mabadiliko. Rais Samia naye ameonyesha kwa vitendo kuwa aina ya kiongozi mwenye kariba hiyo. Haya ni baadhi ya mageuzi yanayotekelezwa kwa weledi mkubwa;
1. Mageuzi katika utekelezaji wa sera ya mambo ya nje hususani katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine.
2. Mageuzi katika uhuru wa Habari na kujieleza hususani sheria zinazosimamia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii.
3. Mageuzi katika uchumi na sera isiyoipa serikali nafasi ya kuhodhi maamuzi ya kibiashara na kuimarisha mazingira ya kuvutia wawekezaji.
4. Mageuzi katika ustahimilivu wa kisiasa na kuimarisha umoja wa kitaifa kama msingi na tunu za Taifa.
5. Mageuzi katika uwazi na uwajibikaji wa Serikali hususani katika mikopo, madeni na mipango ya muda mrefu yenye kugusa maisha ya wananchi.
6. Mageuzi katika dhana ya ustawi wa maisha ya Mwananchi mmoja mmoja na uhuru kamili wa kiuchumi.
7. Mageuzi katika huduma za Jamii, kuhamasisha ubora na unafuu wa gharama za huduma muhimu kama vile Elimu, Afya, Maji, na Miundombinu.
8. Mageuzi katika teknolojia hususani katika kuhimiza na kuwawezesha vijana kuwa sehemu ya jamii inayonufaika na mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR).
9. Mageuzi katika dhana na sera za Kodi hususani katika kuwashirikisha wadau muhimu kwenye maamuzi ya mabadiliko ya Sheria mbalimbali za kodi.
10. Mageuzi ya kiutendaji katika Taasisi za umma. Katika hili tumeona maeneo muhimu kama Jeshi la Polisi yakifanyiwa mabadiliko lakini pia mashirika ya Umma kama vile MSD, TTCL ambayo yanalazimika sasa kujiendesha kisasa na kwa faida.