Mwandishi wetu.
WAGOSI wa Kaya leo wametinga fainali Kombe la Shirikisho kwa ushindi mbele ya Azam katika dimba la Sheikh Amri Abeidn Mkoani Arusha.
Katika mtanange wa dakika 120 za kazi kwa kuwa dk 90 ubao ulisoma Coastal 0-0 Azam FC, na hata zilipoongezwa 30 kukamilisha 120 bado ngoma ilikuwa ni ngumu kwa timu zote.
Mshindi amepatikana kwa mikwaju ya penalti 6-5 huku fainali itakuwa ni Yanga v Coastal Union, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Julai 2.
Mpigaji penalti wa kwanza kwa Azam FC alikuwa ni Lusajo Mwaikenda na penalti yake iliokolewa na Mohamed Hussein na kwa Coastal Union ni Miraj Adam huyu alikosa penalti baada ya kupaisha.