Home SPORTS COASTAL, YANGA KUKIPIGA FAINALI

COASTAL, YANGA KUKIPIGA FAINALI

Mwandishi wetu.

WAGOSI wa Kaya leo wametinga fainali  Kombe la Shirikisho kwa ushindi mbele ya Azam katika dimba la  Sheikh Amri Abeidn Mkoani Arusha.

Katika mtanange wa  dakika 120 za kazi kwa kuwa dk 90 ubao ulisoma Coastal 0-0 Azam FC, na hata zilipoongezwa 30 kukamilisha 120 bado ngoma ilikuwa ni ngumu kwa timu zote.

Mshindi amepatikana kwa mikwaju ya penalti 6-5 huku fainali itakuwa ni Yanga v Coastal Union, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Julai 2.

Mpigaji penalti wa kwanza kwa Azam FC alikuwa ni Lusajo Mwaikenda na penalti yake iliokolewa na Mohamed Hussein na kwa Coastal Union ni Miraj Adam huyu alikosa penalti baada ya kupaisha.

Previous articleRC MAKALA AWATAKA DAR KUWA KINARA WA USAFI
Next articleWANANCHI WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here