Na: Heri Shaaban (Bagamoyo)
WILAYA ya Bagamoyo imejipanga kila mwaka kutoa tuzo sekta ya Elimu Msingi na Sekondari kwa shule zitakazofanya vizuri kitaaluma na ufaulu .
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah, katika kikao cha wadau wa Sekta ya Elimu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Bagamoyo.
“WILAYA yangu ya Bagamoyo mikakati yangu kipaumbele changu Cha kwanza Elimu nimejipanga kutoa tuzo sekta ya eliimu kwa shule zitakazofanya vizuri elimu msingi na sekondari tutakuwa na wiki la juma la elimu katika kilele chake zinatolewa tuzo hizo kwa shule zitakazofanya vizuri” alisema Zainab.
Mkuu wa Wilaya Zainab Abdallah alisema tuzo hizo zitatolewa kila mwaka kwa shule zotakazo fanya vizuri wadau wa elimu na Wanafunzi .
Alisema zawadi hizo zitakazotolewa zikiwemo nyumba na wataalikwa viongozi wa Kitaifa katika makabidhiano hayo Ili kuwapa hamasa kila mwaka waweze kufanya vizuri kitaaluma sambamba na katika MATOKEO yao ngazi ya Kata ,Wilaya ,mkoa mpaka Taifa .
Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Elimu bila malipo hivyo amewataka Wazazi kushirikiana na Walimu na wadau wa Sekta ya Elimu Ili Wanafunzi waweze kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu Wilayani Bagamoyo .
Alisema katika Wilaya ya Bagamoyo KIPAUMBELE chake cha kwanza Wilayani Bagamoyo ni Elimu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza sekta elimu ambapo alitoa pesa za Ujenzi wa madarasa nchi nzima ikiwemo Wilaya Bagamoyo .
Aliwapongeza Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Bagamoyo Wema Kijigile Kwa utendaji wake wa kazi mzuri sekta ya Elimu Msingi pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya hiyo Alois Kaziyareli .
Afisa Elimu Msingi na shule za awali Wema Kijigile alisema kikao chale wamekutana na wadau sekta ya Elimu katika kuzindua mwongozo wa shule ya Msingi na Sekondari sambamba na kusikiliza changamoto za Elimu Kwa ujumla .
Akizungumzia mafanikio Kajigile alisema Kila mwaka inafanya vizuri sekta ya Elimu ambapo mwaka jana MATOKEO ya darasa la Saba imekuwa ya 12 Kitaifa ya tatu kimkoa kwa awamu tatu mfululizo .
Afisa Elimu Sekondari Wilaya Halmashauri ya Bagamoyo , Alois Kaziyareli ,alisema Halmashauri hiyo imekuwa na mwendelezo mzuri katika ufaulu ya mitihani ya Taifa kidato Cha pili Cha nne na sita MATOKEO hayo yameiwezesha Halmashauri kuwa nafasi ya juu Kitaifa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka 2017 mpaka mwaka 2021.
Mwisho.