Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii’ Halmashauri ya Jiji Steven Mushi ,akimkabidhi Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto vikombe vya mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA katika baraza la Madiwani Wilayani Ilala Leo Septemba 07/2022 ambapo katika mashindano hayo Wilaya ya Ilala imefanya visuri(kushoto Naibu Meya SAADY KIMJI (NA HERI SHAABAN ILALA)
Meya wa Haashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto (katikati) akiongoza Dua katika kikao Cha ufunguzi wa Baraza la madiwani Leo Septemba 07/2022 (kushoto )Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji SAADY KIMJI na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo TABU SHAIBU(NA HERI SHAABAN ILALA)
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Dar Salaam Mwalimu Beatrice Edward akizungumza katika kikao Cha Baraza la madiwani Halmashauri hiyo Wilayani Ilala Leo Septemba 07/2022 (NA HERI SHAABAN ILALA).
Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughule akizungumza katika baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Leo Septemba 07/2022 ambapo Diwani Sharik ameililia Halmashauri ijenge Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Wilayani Ilala (NA HERI SHABAN ILALA )
Na : Heri Shaaban (Ilala).
MEYA wa Halmashauri ya Jiji Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, ameagiza Halmashauri ya Jiji hilo kufanya uchunguzi kwa watumishi wake waliosimamishwa katika mradi wa machinjio ya kisasa Vingunguti wafanyiwe uchunguzi wakibainika wachukuliwe hatua kwa kudaiwa kutumia madaraka yao vibaya .
Meya Kumbilamoto aliyasema hayo Dar es Salaam Leo katika BARAZA la Halmashauri hiyo lililo kuwa likijadili na kupitisha Taarifa mbalimbali za Maendeleo ikiwemo Barabara .
“Baadhi ya Wakuu wa Idara wameshindwa kusimamia majukumu yao Serikali imesimamisha mapato katika machinjio Vingunguti baadhi ya Watumishi wakawa wanachukua fedha kwa Mamlaka yao bila kufuata tataribu na kukiuka taratibu za kiutumishi naomba wachunguzwe wakibainika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria “alisema Kumbilamoto
Aliwataka Wakuu wa Idara Halmashauri ya Jiji hilo kubadilika na kufanya kazi kwa weledi Kila moja kusimamia majukumu yake na kutatua kero Kwa wakati .
Wakati huo huo alimpongeza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dkt.Eldhabeth Nyema kwa kufanya kazi kwa weledi na kusimamia miradi yake ya vituo vya Afya vizuri kila Kata ambapo Serikali imeelekeza fedha za Ujenzi wa vituo vya Afya.
Aliwataka Wakuu wa Idara wengine kuiga mfano huo na kuchapa kazi kwa weledi wasifanye kazi Kwa mazoea.
Diwani wa Kata ya Buguruni Busoro Pazi , ameshauri Baraza la Madiwani kuunda Kamati Maalum kuchunguza mradi wa machinjio ya Vingunguti Wilayani Ilala Dar es Salaam kwani anajua siku ya Tarehe ambayo mradi wa ujenzi huo umeanza lakini tarehe ya kumalizika ujenzi wake Madiwani hawajui utaisha lini .
Aliwashauri Watendaji wawe wanafanya ziara kila kata kuangalia changamoto wasikae Ofisini kwani kwenye Kata kuna kero nyingi zinakosa utatuzi kwa wakati .
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar Es salaam Tabu Shaibu kuhusu Watumishi waliosimamishwa kazi katika machinjio ya Vingunguti Halmashauri imeshachukua hatua kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch,Ng’wilabuzu Ludigija alilotoa Septemba 06 mwaka huu baada kufanya ziara katika machinjio ya Vingunguti.
Kaimu Tabu Shaibu alisema Watumishi waliosimamishwa wote wameshaondolewa wanapisha uchunguzi na tayari Halmashauri imeshaweka Watumishi wapya kuanzia Leo Septemba 07 katika machinjio hayo .
Mwisho.