Home BUSINESS SHERIA YA KULINDA DATA BINAFSI KUJADILIWA BUNGENI MWEZI HUU

SHERIA YA KULINDA DATA BINAFSI KUJADILIWA BUNGENI MWEZI HUU

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza Katika mkutano wa wadau wa mawasiliano na TEHAMA (Connect to Connect) Afrika.unaofanyika Kwa siku mbili kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jimmy Yonaz wakifurahia jambo Katika mkutano huo.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jimmy Yonaz wakijadili jambo Katika mkutano huo.

Picha ya pamoja.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye  akiwasili Katika mkutano huo.

DAR ES SALAAM.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Baraza la Mawaziri limeridhia kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi.

Amesema kwa mara ya kwanza sheria hiyo itasomwa bungeni mwezi huu, huku akiwataka wadau watakaokuwa na nafasi za kutoa maoni wafanye hivyo.

Waziri Nape ameyasema hayo leo, wakati akifungua mkutano wa wadau wa mawasiliano na TEHAMA (Connect to Connect) Afrika ambapo amesema ni vyema wadau mbalimbali wakahakikisha wanashiriki kutoa maoni yao juu ya sheria hiyo itakayolinda faragha za mtu katika mawasiliano.

“Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu kuwa na sheria ya kulinda data binafsi na habari njema ni kwamba kwa sasa tumeruhusiwa kuendelea na mchakato na mwezi huu sheria itasomwa bungeni,” amesema Waziri Nape

Aidha Waziri Nape amesema kuwa kama wizara watahakikisha taratibu zote wanazikamilisha kwa wakati ili ziweze kutumika na ni baada ya kupitishwa na Bunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishaisaini.

Waziri huyo amesema kuwa Rais Samia na serikali wamejikita katika kujenga uchumi wa kidigitali ukiwa na lengo la kutomuacha mtu yeyote nyuma.

Katika Mkutano huo wameshiriki wadau mbalimbali wakiwemo watunga Sera, Wadhibiti, Watoa Huduma na wawekezaji huduma za mawasiliano ili kuzijadili na kuzifanyia tathmini ajenda za Kitaifa za Maendeleo na Miradi ya Kuunganisha mtandao wa intaneti kati ya nchi na nchi kote barani Afrika.

Previous articleKAMPUNI YA TIGO, BOOMPLAY KUNUFAISHA WASANII WA MUZIKI NCHINI
Next articleRAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KILICHOKUTANA OFISI NDOGO YA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here