Klabu Ya Jeshi Ya Lugalo Gofu Kuandaa Shindano Kubwa la “TFS Lugalo Open 2022” Litakalofanyika Juni 18 Hadi 19 Mwaka Huu katika klabu hiyo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Klabu Brig. Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema shindano hilo litafanyika kwa mtindo wa Stroke Play Gross na litashirikisha wachezaji wa aina zote huku lengo kuu likiwa ni kuendeleza utumzaji wa mazingira.
Ameongexa kuwa katika mshindano hayo wadhamini wakubwa ni TFS ambao wao wanatoa elimu jinsi ya kitunza mazingira.
Ameongexa kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku ametoa mwito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo.
Naye mmoja wa wadhamini kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Anna Lauwa amesema,wanafurahi kuwa miongoni mwa wadhamini wa shindano hilo na amewataka Watanzania kushiriki katika shindano hilo.
Ameongexa kuwa anafurahishwa kuwa wadau wakubwa katika michuano hiyo ya gofu kwani,huku amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kutembelea misitu pamoja kujitokeza katika mashindano.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu Meja Japhet Masai amesema shindano hilo ni lawazi na litajumuisha Wachezaji wote ambao wamesajiliwa na Klabu zao na ambao wanaviwango vya michezo ambavyo vimehakikiwa na Klabu zao.
Shindano la”TFS Lugalo Open 2022″ linatarajiwa kufanyika Juni 18 hadi 19 ambapo mgeni rasmi katika ufungaji wa shindano hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makala.