Aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya kilichotokea leo tarehe 07 Mei, 2025 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
kufuatia kifo hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku 7 za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo tarehe 7 hadi 13 Mei, 2025.
Taarifa zaidi ya Mipango kamili ya msiba itaendelea kutolewa na Serikali.
Rais Dkt. Samia anawapa pole Ndugu, jamaa na Watanzania wote kwa msiba huu.