Home LOCAL UANDISHI WA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO UNAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA NCHINI

UANDISHI WA HABARI ZINAZOHUSU WATOTO UNAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA NCHINI

Na kwamba, taarifa nyingi zinazowahusu watoto kwenye vyombo vya habari, huwa hazioneshwi ama kuripotiwa muendelezo wake hivyo kusababisha matukio mabaya kuendelea kutokea.

Hayo yameelezwa mjini Morogoro katika mafunzo kwa wakuu wa vitengo vinavyosimamia wanafunzi wa uandishi wa habari katika vyuo mbalimbali nchini.

Kwenye mafunzo hayo, Dk. Darius Mukiza, Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Undishi wa Habari amesema, bado kiwango cha habari za watoto kipo chini nchini.

‘‘Pamoja na kwamba habari zinaripotiwa, mchakato wa habari hizo huacha mambo mengi na wakati mwingine habari hizo zinakosa muendelezo.

‘‘Hii ina maana kwamba, vyombo vya habari havihitaji tu kuripoti kwa haki, uaminifu na usahihi juu ya uzoefu wa utoto, lakini lazima pia kutoa nafasi kwa maoni mbalimbali, rangi na ubunifu ya watoto wenyewe na dharura za afya,’’ amesema Dk. Mukiza.

Paulo Mabuga, Mtaalamu wa Vyombo vya Habari kutoka Mwanza amesema, mwongozo kwa walimu wa waandishi unastahili kuandaliwa kwa ustadi kwa kuwa, ndio wanwaandaa waandishi wa kesho.

‘‘Kwa hakika hivi karibuni niliangalia chombo kimoja cha habari, namna walivyoripoti habari ya tukio la mtoto mmoja, inasikitisha. Mwandishi alishindwa kupanga picha, kutoa maelezo na mwisho wa taarifa ile haikuwa na ujumbe wenye athari,’’ amesema Mabuga.

Nassoro Ali, Mkuu wa Kitengo cha Uandishi wa Habari Chuo Kikuu cha Waislam Morogoro (MUM) amesema, kuna haja ya kuwaandaa wanafunzi kuyakabili mazingira ya uandishi wa habari za watoto za uchunguzi.

Diana Msovu kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Idara ya Undishi wa Habari amesema, kuna kila sababu ya kuimarisha uandishi wa habari za wanawake.

‘‘Nchini kwetu bado uandishi wa habari za namna hii upo chini, unapoangalia uwasilishwaji wa taarifa hizi katika nchi nyingine ndio utabaini utofauti.

‘‘Hili linapaswa kuwanza vyuoni kwa wanafunzi, kila habari ina umuhimu wake hivyo zote zinapaswa kuandikwa kwa uzito unaofanana,’’ amesema.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), limeendesha mafunzo hayo ya siku tatu kwa lengo la kuwajengeo uwezo walimu ambao ndio wanasimaia wanafunzi wa waandishi wa habari katika vyuo vyao.

‘‘Mafunzo haya ni muhimu kwa kuwa, nyinyi ni walimu tena ndio waandaaji wa waandishi, ni vizuri kujengewa uwezo wa namna ya kuandika habari zinazoweza kubadilisha taswira kwa watoto.

‘‘Tunafanya hivyo kama mlivyoeleza wenyewe kwamba, taarifa za wanahabari kuhusu habari za watoto zina kasoro nyingi kuanzia uandaaji wa picha, mpangilio na maelezo yanayotolewa,’’amesema Neville Meena msimamizi wa mafunzo hayo.

Previous articleDC ILALA AWAPONGEZA WENYEVITI WA MITAA, MABALOZI WA SHINA KWA KUTOA USHIRIKIANO ZOEZI LA SENSA
Next articleJAPAN YAAHIDI KUTOA DOLA BILIONI 30 KUZISAIDIA NCHI ZA AFRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here