rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wallace Karia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa marudiano wa mkondo wa pili wa robo fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Masri utakaopigwa Aprili 9, 2025 katika dimba la Benjamin Mkapa.
Meneja wa Mawasiliano wa klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simb SC Amed Ally, amethibitisha hilo alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Kispika le leo Aprili 4, 2025, Jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa timu yao ina kila sababu ya kumpa heshma hiyo Karia kwa kutambua mchango wake katika soka la Tanzania.
“Tuna kila sababu ya kumpa nafasi hii kwa kutambua mchango wake. Tunatambua, tunaheshimu mchango wa Wallace Karia kwenye mpira wa Tanzania. Simba SC kufika nafasi ya sita kwa ubora Afrika ni katika uongozi wa wake.” amesema Ahmed Ally.