Home INTERNATIONAL 4R’s ZA RAIS SAMIA ZAITIKISA GENEVA

4R’s ZA RAIS SAMIA ZAITIKISA GENEVA

GENEVA 

Akizungumza  wakati akiiwakilisha Nchi ya Tanzania katika Kikao cha 58 Cha Haki za Binadamu kinachofanyika Geneva Nchini Uswisi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Dr. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa,   Nchi ya Tanzania imeendelea kuweka kipaumbele katika uendelezaji na ulinzi wa Haki za Binadamu katika utekelezaji wa shughuli za Serikali.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Waziri Ndumbaro amesema  kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 na Katiba ya Zanzibar, 1984, Tanzania  imeendelea kusimamia Utu wa Kibinadamu kwa mujibu wa  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu na inaendana na mkakati uliopitishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ambao umejikita katika 4Rs kuwa ni Maridhiano, Uthabiti,Mageuzi na Kujenga upya.

Akiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa Haki za Binadamu katika Hifadhi ya Ngorongoro, Waziri Ndumbaro amesema kuwa Serika ya Tanzania imeendelea kuweka uwiano sawa wa  Haki za Binadamu na Maisha kwa kuzingatia uhifadhi.

Waziri Ndumbaro amefafanua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusimami Haki za Binadamu Ngorongoro alikutana na Viongozi wa Vijiji na Kimila na kusikiliza kero zao na kuanzisha Tumbe mbili za Ushauri, kushauri masuala ya Ardhi na kushauri kuhusu Mpango unaoendelea wa kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro kwenda Msomera.

Aidha, Waziri Ndumbaro ameongezea lengo la jitihada hizo ni kuhakikisha zoezi la hiari linafanya kazi kwa urahisi na kwamba kero za Wananchi zinashughulikiwa

Maeneo mengine ya usimamizi wa Haki za Binadamu yaliyowasilishwa katika Mkutano huo ni pamoja na kufanya Uchaguzi Huru na Haki kila baada ya miaka mitano,Uhuru wa Vyombo vya Habari na kujieleza,kulinda Haki za makundi hatarishi ukiwemo ustawi wa Watu Wenye Ualbino na Usaidizi kwa Watu wenye Ulemavu.