
Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za usafirishaji mtandaoni nchii na Barani Afrika imefurahishwa na kuongezeka kwa idadi ya wateja wanaotumia huduma hiyo.
Dimmy Kanyankole ni Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya alisema kuwa kuongezekwa kwa idadi ya wateja inatokana na huduma nzuri zitolewa na Bolt na zenye uhakika ambapo hayo yalithibitika siku ya wapendaao Valentine.
“Siku ya Valentine wateja waliotumia Bolt ilikuwa ni kubwa na hiyo imetokana naa huduma zenye uhakika zinazotolewa na kampuni hiyo haya hivyo,”ameema meneja.

Alisema kuwa kama kampuni inayoongoza kwa usafiri wa kidijitali Tanzania, Bolt ilitarajia ongezeko kubwa la mahitaji ya safari kuelekea maeneo maarufu ya Dar es Salaam ambapo Bolt ilichukua hatua kuhakikisha usafiri unaoendelea na wa bei nafuu kwa wote.
“Hatua yao ya kwanza ilikuwa kutangaza usafiri huo kwenye itandao ya kijamii na kutoa ofa ya punguzo la asilimia 40 iliyoisha 15 Februari 15, saa 1:00 asubuhi.
“Kilichofanya Siku ya Wapendanao iwe maalum zaidi mwaka huu mwingiliano usio wa kawaida wa maombi ya safari, pamoja na idadi ya rekodi ya safari zilizofanyika usiku huo tunawashauri kuwa uwe endelevu kwani huduma za usafiri zina nafasi muhimu katika uchumi” alisema Kanyankole, Meneja Mkuu wa Bolt Tanzania na Kenya
Aliongeza kuwa kama biashara yenye nguvu, Bolt inaweza kuchochea mahitaji makubwa na kufungua matumizi ya wateja katika migahawa, vituo vya burudani, na maeneo mengine ya uchumi.

Huduma za usafiri wa mtandao zinachukua takriban asilimia 25–30 ya safari za mijini katika vituo vikuu kama Dar es Salaam
Kwa mujibu wa ripoti ya Desemba 2023 iliyotolewa na REPOA kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Oxford, zaidi ya watu 10,000 wanafanya kazi katika sekta ya huduma za usafiri wa mtandao kama madereva wa teksi, pikipiki, na traisikali, pamoja na zaidi ya 3,000 katika huduma za usafirishaji.
Idadi hizi zinaendelea kukua ili kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka, zikileta ongezeko linalolingana katika uhai wa uchumi kama ilivyotarajiwa wakati wa Siku ya Wapendanao.