Home LOCAL WASSIRA: UZEE SIYO HOJA, BADO NINA UWEZO

WASSIRA: UZEE SIYO HOJA, BADO NINA UWEZO

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wassira, akizungumza na viongozi Wananchi   katika Kata ya Kakubilo, Wilaya ya Geita mkoani Geita  leo Januari 29, 2025  Katika Uzinduzi wa kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 48 ya kuzaliwa CCM Mkoani GEITA.  (Picha na CCM )

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

WANANCHI wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kakubilo, Wilaya ya Geita mkoani Geita Katika Uzinduzi wa kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 48 ya kuzaliwa CCM Mkoani GEITA.  (Picha na CCM ).

…….

Na Mwandishi Wetu,
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema hakitayumbishwa na hoja dhaifu za upinzani kuhusu maendeleo huku ikiutaka upinzani kujipanga vema kuhimili kishindo chake.Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM – Bara, Stephen Wasira ametoa angalizo kwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaotaka kutumia hoja ya umri wake kama mtaji wa kisiasa na kuwataka wajipange vyema.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kakubilo wilayani Geita Mkoa wa Geita, leo, Wasira alisema CCM imejipanga kwa kila namna kuwaletea maendeleo wananchi na haitayumbishwa na hoja dhaifu.

“Wako watu wanahoji na kusema tumekaa miaka mingi madarakani, hii ni hoja dhaifu kwani tulipokuwa tunapigannia uhuru tuliingia mkataba wa kukaa madarakani kwa muda gani.

“Nataka tuwaambie kuwa bado tutakaa sana madarakani, hatuna mpango wa kutoka kwa kuwa tunaongoza kwa ridhaa ya wananchi,”
alisema.

HOJA YA UMRIAlisema viongozi wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wake Tundu Lissu na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche kwamba Wasira ni mzee, hiyo ni hoja dhaifu kwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kiutendaji hususan katika siasa.

“Ukiona mtu anasemasema ujue sindano imemfikia. Hatuwezi kubishana na kibaka.

“Tunakwenda na Falsafa ya 4R ambazo muasisi wake ni Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Njooni tuzungumze hatuwezi kubishana,”
alisema.

Alisema CHADEMA na viongozi wake walipewa nafasi ya kukaa na kujadili mambo mbalimbali kuhusu mustakbali wa maridhiano.

“Chadema wasilisha hoja 11, la kwanza walitaka wanachama wao waliokimbia nchi warudi nchini akiwemo Tundu Lissu ambaye alirejea nchini.

Jambo lingine ni kuhusu wanachama wa chama hicho ambao walikuwa na kesi mbalimbali akiwemo Lissu na wengine walikuwa wamefungwa jela ambapo walitoka kwa msamaha wa rais.

“Pia, walitaka kuruhusiwa mikutano ikaruhusiwa na wakaja mpaka huku lakini hawakuwa na jambo.

“Jambo ambalo lilishindikana ni kuwafukuza wabunge wa viti maalumu ambao jambo lao liko mahakamani,”
alisema

Wasira alisema jambo lingine ni kuhusu katiba mpya ambapo walitaka iandike kwa siri “sisi tukasema hatuwezi kufanya siri jambo la wananchi na hapo ndipo tulipoishia wakaamua kutoka tena kwa hiyari sasa waliingia kwa hiyari wametoka kwa hiyari.”

Alisema licha umri wake mkubwa lakini na uwezo na kwamba umri mkubwa sio kigezo cha kushindwa kuwajibika.

“Wakaulize Wamarekani hivi karibuni walifanya uchaguzi na wamerekani wakaamua kumchagua Trump ambaye ana umri km wangu wakamuacha Camara ambaye ana miaka 60,”
alisema.

Alisema ‘wao wanadhani mawazo ni umri “mimi nina umri mkubwa lakini nina mawazobya miaka 55 na gari ni injini siyo bodi, kama anataka ushahidi aende Muhimbili au India.”