1️⃣ Mshindi wa Kwanza; Taasisi inayolipa kodi kubwa na inayozingatia misingi na kanuni bora za ulipaji kodi (sekta ya kibenki).
2️⃣ Mshindi wa Kwanza; Mchangiaji bora wa ukusanyaji kodi nchini.
3️⃣ Mshindi wa kwanza; Taasisi inayolipa kodi kubwa zaidi nchini na kuzingatia kanuni za ulipaji kodi (sekta zote nchini).
Tuzo hizi zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kwenye Siku ya Shukrani na tuzo kwa Mlipa Kodi na kupokelewa kwa niaba ya Benki na Afisa Mtendaji Mkuu wetu, Bi. Ruth Zaipuna.
Mafanikio haya kwa benki ya NMB ni matokeo ya kuzingatia kanuni bora za ulipaji kodi, ufanisi katika kujiendesha na ubunifu wa suluhishi bora za kifedha zenye manufaa kwa Wateja na Taifa letu.
Dhamira yao ni kuendelea kuendesha biashara ya kutoa huduma za fedha kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchi ili kuchangia kikamilifu ujenzi wa uchumi wa Tanzania.