Na, Lilian Ekonga
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limerangaza Matokeo ya mtihani wa kuhitimu kidato cha Nne uliofanyika mwezi Novemba mwaka ja a yameta, huku ufaulu ukiongezeka kwa Asilimia 5.54.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania-NECTA, Dokta Said Mohamed, ametangaza matokeo hayo jijini Dar es salaam, akisema watahiniwa wa shule waliopata ubora wa ufaulu katika madaraja ya I-III, kwa mwaka 2024 ni 221,953 sawa na asilimia 42.96.
Mwaka 2023 watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja ya I-III walikuwa 197,426 sawa na asilimia 37.42, hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 5.54 ikilinganishwa na mwaka 2023.
Ubora wa ufaulu wa madaraja ya I-III, Dokta Mohamed, amesema ni mzuri zaidi kwa wavulana ikilinganishwa na wasichana, ambapo wavulana ni 119,869 sawa na asilimia 48.90 na wasichana 102,084 sawa na asilimia 37.59 ya wasichana wote wenye matokeo.
Ameongea kuwa mahudhurio ya mtihani huo yalikuwa asilimia 97.76 sawa na watahiniwa 517,460, huku watahiniwa 11,869 sawa na Asilimia 2.24 hawakufanya mtihani.
Aidha baraza limefuta matokeo yote ya Watahiniwa 67 waliobainika
kufanya udanganyifu na Watahiniwa watano walioandika lugha ya matusi katika skripti zao katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika November 2024 ambapo matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani Mwaka 2016.
Amesema Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia pia kutoa matokeo ya Watahiniwa 459 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne, 2024 kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo na Watahiniwa husika wamepewa fursa ya kufanya Mtihani kwa masomo ambayo hawakuyafanya kwa sababu ya ugonjwa mwaka 2025 kwa mujibu wa Kifungu cha 32(1) cha Kanuni za Mitihani.
Katika hatua nyingine Baraza la Mitihani la Tanzania limefungia kituo cha P6384 BSL Open School
kilichopo Mkoa wa Shinyanga kuwa kituo cha Mitihani ya Taifa kutokana na kuratibu mipango ya udanganyifu hadi hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa.
http://UFAULU KIDATO CHA NNE 2024 WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 5.54