Home LOCAL KISARAWE  KUSHEREHEKEA  BIRTHDAY  YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUKATA KEKI

KISARAWE  KUSHEREHEKEA  BIRTHDAY  YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWA KUKATA KEKI

Mkuu wa Wilaya  ya Kisarawe  Petro Magoti  amesema  maandalizi  ya kusherehekea  siku ya mfanano wa tarehe  ya kuzaliwa rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  ifikapo  tarehe 27  Januari  2025
Akizungumza na wanahabari mapema leo, Januari, 22 ,2025 amesema kuwa wamejipanga kusherehekea  ‘birthday” ya Rais  hodari  na  mchapakazi  na kutawa na tutakata keki na kusherehekea  pamoja na wananchi wa Kisarawe huku wakimuimbea dua njema kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa afya  na umri ili aweze  kulitumia taifa lake.
“Tuna Rais hodari, shupavu,na mchapakazi hivyo basi sisi Wanakisare tutasherehekea siku hiyo kwa kukata keki na tutakula kwa pamoja,hivyo nawakaribisha Wananchi wote wa Kisarawe, amesema Magoti
Aidha DC Magoti amesema kuwa Januari 25 asubuhi  kutafanyika uzinduzi  wa  wiki ya sheria utakaofanyika kwenye uwanja wa Chanzige Wilayani  Kisarawe Mkoa wa Pwani ambapo huduma ya kisheria  itaendeshwa kwa juma moja huku kilele chake kitafanyika Februari mosi .
Huduma za Kimahakama zitafanyika kwenye Kata zote za Kisarawe  wananchi ambao wanakabiliana na migogoro  ya ardhi, mirathi, ndoa na mengineyo wameombwa kujitokeza kupata huduma hiyo.ambayo itaanza saa moja asubuhi hadi jioni
Pia DC Magoti ametoa onyo  kali kwa wazazi  hawawapeleki watoto  shuleni bila ya kuwa na sababu maalumu kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Naye Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama  ya Kisarawe  Mhe.Emmy Amon Nsangalufu amesema  kuwa wiki ya sheria  itatolewa tarehe 25 hadi 31  Januari  mwaka huu pia kutakuwa na gari ambalo litakuwa mfano wa  Mahakama  inayotembea huku lengo likiwa kuwafikia wananchi na kuwapa huduma wanayostahili.
Nsangalufu ametoa wito kwa wananchi kuwa Mahakama  ni mali ya wananchi hivyo waitumie kwa manufaa yao  na siku ya uzinduzi  wataanza na maandamano asubuhi  kwenda kukutana Uwanja wa Chanzige.
” Tumejipanga kuwafikia wazee na watu wote wasiojiweza ndani ya kata zote  17 tutakuwa na gari pamoja na Mawakili wabobevu katika kutatua shida zao” amesema Nsangalufu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here