Home LOCAL KISHINDO CHA RAIS SAMIA SEKTA YA UTALII CHASIKIKA KILWA

KISHINDO CHA RAIS SAMIA SEKTA YA UTALII CHASIKIKA KILWA

Mataifa mbalimbali yafurika Hifadhi ya Urithi wa Dunia Kilwa Kisiwani

Na Beatus Maganja, Kilwa.

Kazi kubwa ya kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu duniani iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kudhihirika na kishindo chake kutikisa katika Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia ya Magofu ya Kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo inaendelea kupokea makundi ya watalii wa nje kutoka Mataifa mbalimbali.

Hifadhi hiyo iliyo chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imefungua ukurasa mpya wa mwaka 2025 Kwa kupokea watalii wa kigeni kutoka Mataifa mbalimbali ambapo Januari 18, 2025 ilipokea wageni 98 na leo Januari 22, 2025 imepokea Kundi lingine la watalii wapatao 173 kutoka Mataifa ya Uingereza,Finland, Sychelles, Marekani, Sweden, Australia na Ireland ambao Kwa kutumia meli kubwa aina ya Hebridean Sky walifika hifadhini humo Kwa lengo la kutalii.

Hatua iliyochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kucheza filamu ya Royal Tour iliyokuwa na lengo la kuhuisha Sekta ya Utalii nchini iliyokuwa imefifishwa na janga la UVIKO 19, janga linalotajwa kusababisha mdororo wa uchumi duniani imesaidia kuchechemua Sekta ya utalii nchini na kuifanya TAWA kuwa mojawapo ya taasisi za kiuhifadhi zilizonufaika Kwa kupata Idadi kubwa ya wageni wanaotembelea katika maeneo inayosimamia kwa shughuli za utalii wa picha na uwindaji wa kitalii.

Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha Mwaka 2023/24 TAWA kupitia Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara iliweza kupokea meli 9 za kitalii na jumla ya watalii wa Kigeni 1,047.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here