Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni NewTan Insurance, Nelson Rwihula akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kutambulisha jina jipya la Kampuni hiyo la NewTan, uliofanyika leo Januari 20, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi, kampuni ya NewTan Insurance Moses Obonyo, akizungumza alipokuwa akifungua mkutano huo, uliotambulisha jina jipya la Kampuni la NewTan Insurance, kutoka jina la zamani la UAP Insurance, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA;HUGHES DUGILO
DAR ES SALAAM
Watanzania hususani wanaojihusisha na kilimo wameshauriwa kuweka utaratibu wa kukata Bima itakatayowezsha kulinda mazao yao na kujikinga wakati wa majanga yanayoweza kuharibu mazao yao.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, uliofayika leo Januari 21, 2025,Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni inayojihusisha na masuala ya Bima NewTan Insurance, Nelson Rwihula amesema wakulima wamekuwa wakikabiliwa na majanga mbalimbali na kujikuta wanapata hasara kubwa kutokana na kukosa Bima inayoweza kulipa fidia mazao yao.
Ameeleza kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni ukosefu wa elimu ya Bima, nakwamba kampuni hiyo imejipanga kutoa elimu kwa wadau waliopo katika sekta hiyo.
“Kuna majanga mkulima anakuwa nayo kila siku, yakiwemo magonjwa, wadudu waharibifu, ukame na na mvua kubwa ambazo azizuiliki, yote haya yanahitaji Bima ili mkulima ajihakikishie usalama wake na mazao yake wakati wote.
“Sisi tunaangalia Ile hasara aliyoipata tunaenda kumlipa fidia” amesema Rwihula
Kwa upande wake Meneja wa Biashara za Benki wa Kampuni hiyo Frank Kajo, amesema wanaungana na Serikali katika kuwahimiza wakulima kuwa kwenye vikundi mbalimbali, na kujiunga kwenye vyama vya ushirika Ili kuwafikia kwa urahisi na kuwahudumia.
Ameongeza kuwa elimu ya Bima inaweza kufika kwa urahisi zaidi kupitia vyama vyao vya ushirika na vikundi kwa kupitia matawi yao yaliyopo mikoani pamoja na mawakala wao.
Katika Mkutano huo Kampuni hiyo yenye matawi tisa nchini, imetangaza jina jipya ambalo kwa sasa itaitwa NewTan Insurance badala ya jina la zamani la UAP Insurance, nakwamba mabadiliko hayo hayataathili utendaji wao wakazi kwani huduma zao zitaendelea kuboreshwa.