Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO 8882 na PMO 8882 2 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika baada ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda kufungua Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wakisikiliza wimbo wa taifa wa Uganda katika ufunguzi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. Waziri Mkuu alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wenye mkutano huo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Rais Yoweri Museveni wa Uganda (wa nne kushoto) pamoja na viongozi wengene wakifuatilia hotuba ya Waziri Kassim Majaliwa aliyoitoa wakati alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda,Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort Munyonyo, Kampala Uganda, Januari 11, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
*Rais Museveni asifu bora wa mchele wa Tanzania, asisitiza kushindana kwa ubora
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewaeleza Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha masuala ya utafiti na kushirikisha sekta binafsi, taasisi za umma zinazojishughulisha na kilimo ili kuhakikisha nchi inakuwa tegemeo katika uzalishaji wa chakula barani Afrika.
Mheshimiwa Majaliwa amesema viongozi wa nchi za Afrika wameonesha matumaini makubwa na mikakati iliyowekwa na Tanzania katika kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora hasa mpunga na mahindi. “Haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo nchini.”
Waziri Mkuu amesema Serikali imefarijika kusikia baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika akiwemo Mheshimiwa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni wakiisifia Tanzania kwa kuzalisha mazao ya chakula yenye ubora na hasa mpunga na mahindi. “Haya ni mafanikio makubwa katika sekta ya kilimo nchini.”
Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 11, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Umoja wa Afrika wa kupitisha Programu ya Kuendeleza Kilimo Barani Afrika (CAADP 2026 – 2035) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala nchini Uganda.
“Natamani watu washindane kwa ubora katika uzalishaji, mfano mchele wa kutoka Tanzania ni bora zaidi na gharama yake ipo chini, kuna wakati walitaka nizuie usije lakini nikawataka nao wajitahidi kushindana katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora.” Kauli ya Mheshimiwa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni aliyoitoa wakati akiwasilisha hotuba yake katika mkutano huo, inatoa fursa kwa mataifa mengine kununua mchele kutoka Tanzania.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Tanzania imeweka mkakati wa kuhakikisha inaendelea kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya ndani na kuuza ziada nje. “Kwa sasa kilimo chetu si cha kujikimu bali ni cha kibiashara.”
Awali, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza ili kuongeza tija na kukuza ajira hususan kwa vijana.
Ametoa mfano wa zao la kahawa, ambapo nchini Uganda kilo moja ya kahawa ghafi inauzwa dola mbili za Marekani, ambapo kahawa hiyo hiyo ikichakatwa bei inaongezeka na kuuzwa dola 40 za Marekani.
“Tunapoteza ajira na fedha nyingi katika mazao ya kilimo kwa kuyauza kabla ya kuchakatwa. Lazima tuongeze thamani ya mazao yetu na inasikitisha kuona nchi za Afrika zikiendelea kuuza malighafi, lazima tubadilike.”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat amesisitiza ushirikishwaji wa vijana katika sekta ya kilimo na kuweka mikakati thabiti ya kuyawezesha mataifa hayo ya Afrika kuzalisha chakula cha kutosha.
“Kwa nini Afrika bado tuna njaa wakati tuna ardhi ya kutosha, tuhusishe vijana katika kilimo kwani usalama wa chakula na lishe bado haujabadilika kwa sababu wengi wetu bado tunakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula na lishe bora. Hivyo tunatakiwa kubadilika.”
Naye, Waziri wa Nchi wa Norway na Mwakilishi wa Wadau wa Maendeleo, Bjørg Sandkjaer amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto ya kuwafikia walengwa, hivyo amewahakikishia viongozi hao kuwa wataendelea kushirikiana nao kuhakikisha Tamko la Kampala linakwenda kuleta ustahimilivu katika upatikanaji wa chakula na lishe bora barani Afrika.
Katika mkutano wa utangulizi Mawaziri wa Sekta ya Kilimo walipitisha Mpango unaofuata wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Barani Afrika ambao umejikita kwenye mifumo jumuishi ya uzalishaji wa chakula kwa kuzihusisha Sekta nyingine zinazochangia kwenye uzalishaji wa chakula ikiwemo miundombinu, elimu na afya.
Aidha, msimamo wa Tanzania kwenye kupitisha Mpango huo ulikuwa ni kuhimiza nchi wanachama kuichukulia Sekta ya Kilimo kwa mapana yake ili kuwa na uhuru wa chakula (food sovereignty) na kila nchi wanachama kuendelea kuwekeza kwenye Sekta ya Kilimo kwa upana wake pasipo kuathiri mazingira.
Viongozi wengine kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo –Zanzibar, Shamata Shaame Khamis, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dennis Londo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti.