Home LOCAL RC SHIGELLA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA ALIYEKUWA RC WA GEITA ROSEMARY SENYAMULE

RC SHIGELLA AKABIDHIWA RASMI OFISI NA ALIYEKUWA RC WA GEITA ROSEMARY SENYAMULE

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Rosemary Senyamule ambae sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Dododoma

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita prof. Godius Kahyarara

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella

Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella na Mkuu wa Mkoa wa Dododoma wakati wa makabidhiano ya ofisi

Na. Costantine James, GEITA

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Martin Shigella amewahidi wakazi wa Geita kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia misingi na taratibu za kiutumishi kwa lengo la kuleta maendeleo katika mkoa huo.

Mhe, Shigella amesema hayo katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi baina yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Dododoma.

Shigelka amesema anatambuwa dhamana kubwa aliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Sulihu Hassan hivyo hanabudi kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya utu pamoja na kushirikiana kwa pamoaja na watendaji wa serikali katika mkoa wa Geita.

“Nikupongeze kwanza kwa kuteuliwa tena na Mh Rais kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,,pia ni waahidi wanageita nitafanyakazi kwakuzingatia misingi ya utu kwa kushirikiana na watendaji wa serikali “amesema RC Shigella .

Katibu tawala wa Mkoa wa Geita Professa Godius Kahyarara amesema kipindi kifupi ambacho wamefika Mkoani hapa wamebaini uwepo utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu .

“Mimi na Rc wangu tumefika Geita kwa kipindi hiki kifupi tumebaini uwepo wa utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu “amesema profesa Kahyarara .

Naye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Rosemary Staki Senyamule ambae kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Dododm amesema kitendo cha Mh Rais kumwamini na kumteuwa tena kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma ni kutokana na heshima kubwa na ushirikiano waliokuwa akipewa na watendaji wake ,Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri ,Madiwani katika kusimamia miradi ya maendeleo .

“Napenda kumshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniteuwa tena na kunipeleka Mkoa wa Dodoma kuwatumikia wananchi ,nimeacha nimepandisha maonesho ya teknolojia ya Madini kutoka kuwa ya kimkoa na kuwa maonesho ya kimataifa”amesema RC Senyamule.

Previous articleMASHINDANO TEMBO CUP 2022 YATIKISA ITIGI-TIMU ZA KITARAK FC, DOROTO FC, SANJARANDA FC NA MUHANGA FC ZAINGIA NUSU FAINAL
Next articleWATENDAJI WA SENSA WATAKIWA KUFANYAKAZI KWA BIDII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here