Home LOCAL POLISI WATOA UFAFANUZI KUMHUSU MCHEZAJI MORRISON

POLISI WATOA UFAFANUZI KUMHUSU MCHEZAJI MORRISON

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi lingependa kutoa ufafanuzi wa taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kumhusu Mchezaji Bernard Morrison ikituhumu Kituo cha Polisi Mbweni.

Taarifa hiyo kila mtandao unaongeza chumvi kutokana na kuwa na taarifa ya upande mmoja.

Ufafanuzi ni kwamba, Bernard Morrison, Machi, 2024 alifungua kesi ya Wizi wa Kuaminiwa katika Kituo cha Polisi Mbweni kuwa, akiwa Ghana alimtumia Abdul Rakeeb Mgaya kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) ili amkabidhi mdogo wake aliyemtaja kwa jina la Boat anayeishi hapa nchini akitafuta timu itakayo msajili lakini hakufanya hivyo.

Baada ya malalamiko hayo aliyetuhumiwa alitafutwa na alipohojiwa alieleza ni kweli alitumiwa hizo fedha ili zisaidie kwenye gharama za kumsajili huyo mdogo wake lakini ilishindikana kwasababu hakuwa na kiwango cha kusajiliwa na timu aliyokuwa anahitaji. Hata hivyo, alimtaka Bernard Morrison ampe muda atamrejeshea fedha zake.

Pia alielezwa kulingana na ushahidi hakuna kesi ya jinai. Hivyo walielewana na kwa vile wote ni raia wa Ghana walikubaliana kulipana.

Juni 3,2024 iliripotiwa kesi ya kuharibu mali ambapo Bernard Morrison akiwa na mdogo wake na mtu mwingine walifika katika nyumba anayoishi Abdul Rakeeb na kuvunja geti kisha kuchukuwa kwa nguvu gari aina ya IST namba T239 DFM.

Bernard Morrison aliendelea kutafutwa bila mafanikio lakini Abdul Rakeeb walifanikiwa kuliona gari hilo likiwa limeegeshwa sehemu na kulichukuwa na kulipeleka Kituo cha Polisi Mbweni.

Hivyo Bernard Morrison anachotakiwa kufanya ni kuacha kujificha, kusema ukweli na kufika kituo cha Polisi kuonana na uongozi ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na: David A. Misime – DCP Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu ya Polisi Dodoma,Tanzania

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here