Home LOCAL TASAF YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUWA MKOMBOZI KWA WANANCHI WANYONGE

TASAF YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUWA MKOMBOZI KWA WANANCHI WANYONGE

Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongizi wakuu wa Kitaifa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kwa kuendelea kuwa wakombozi kwa wananchi wanyonge wa Tanzania kwa upande wa Bara na Visiwani.

Machano Ali Machano, aliyasema hayo jana wakati kamati hiyo ilipotembelea katika eneo la Mradi wa kuzalisha inzi chuma Mabwepande jijini Dar es Salaam.

Amesema juhudi hizo ni za kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia umasikini wananchi wote wa Tanzania.

“Kipekee tuwashukuru sana ndugu zetu wa TASAF kwa sababu karibu asilimia 80 ya wajumbe wa kamati hii hawajawahi kufika eneo hili la Mabwepande.

“Lakini sio kufika tu, tumeshuhudia miradi ambayo hatujawahi kuiona hongereni sana kwa kuamua kutuleta hapa.

“Lakini hapa tumeshuhuda muendelezo wa vikundi lakini na wale ambao tayari wamehitimu kutoka TASAF na leo hii wameanza kujitegemea, tumeona mashuhuda watatu wakijieleza namnagani mmewakomboa kutoka katika umasikini.

“Wengine wamekiri wenyewe kwamba vijana wao sasa wako chuo kikuu wanaendelea na masomo hongereni sana,”amewapongeza Machano.

Mmoja wa wanufaika  Sina Nasor Said ambaye ni Katibu wa Kikundi cha kuzalisha funza na Katibu wa Vikoba, alisema walikabidhiwa mradi huo mwaka 2021 huku akisema wanaufurahia na kuupenda pia.

“Tunazalisha funza “Inzi Chuma”kupitia takaoza yani maganda ya viazi, ndizi, ubwabwa, nyama kasoro maganda chachu ambayo ni Ndimu, Nanasi na Malimau au mifuko ya Palastiki hayo hayahusiki.

“Baada ya kuweka maganda kwenye kizimba ndani ya wiki moja inzi chuma wanakuja kutaga mayai, wanavyo taga mayai wanatoa wadudu kama hawa funza.

Hawa funza baada ya wiki mbili wanakuwa wachanga wakikomaa sasa wateja wanachagua wanataka wa aina gani wasamaki, wang’ombe au nguruwe au kuku hujichagulia wanaofaa kwa chakula cha mifugo yao,”amesema Sina Said.

Sina mesema changamoto yao kubwa upatikanaji wa takataka na gharama za usafiri kama tungezipata kirahisi na kwa gharama ndogo ya usafiri wangefurahi zaidi.

“Tangu tumeanza kushughulika na mradi huu kiukweli tumenufaika sana kwa sababu hadi sasa tumepata kiasi cha Sh. 200,000 na zaidi tunapata hela na tunakopeshana kwenye vikoba,”amesema.

Awali akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya kusimamia ofisi za Viongizi wakuu wa Kitaifa Zanzibara  Tumpe Lukongo – Mtaalamu wa Tafiti TASAF mesema kwa majaribo kikundi kiliweza kuzalisha na kufanikiwa kuuza kupitia ule mradi wa takataka na kupata fedha za kujikimu huku nyingine waliziweka kwenye kikundi chao kama faida.

“Lakini pia waliweza kujitafutia masoko na wao wanatudhihirishia kwamba wanaweza kuendesha mradi kama huu na manispaa nyingine zinazofanana na Mabwepande zenye uchafu mwingi ili kuweza kufanikiwa kufanya mazingira yawe safi lakini pia kutengeneza uchumi kupitia hao funza,”amesema.

Previous articleSELEMAN MSUYA:RITA WAMALIZA MGOGORO WA MSIKITI WA IJUMAA MWANZA.
Next articleBILIONEA MULOKOZI ANUNUA NDEGE BINAFSI, ATUA MANYARA ,WANANCHI WAFIKA KUMPOKEA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here