Na. Elimu ya Afya kwa Umma .
Wananchi kutoka maeneo mbalimbali katika Jimbo la Peramiho wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jenista Mhagama kwa kuanzisha Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika Mkoa wa Ruvuma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wananchi hao wamesema Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii wana mchango mkubwa kwani kupitia Mpango huo elimu ya Afya watakuwa wanapata kwa urahisi zaidi karibu na maeneo yao.
“Nashukuru sana Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Mpango huu wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii eneo la Peramiho na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pia nimshukuru Waziri wa Afya na Mbunge wangu wa Jimbo la Peramiho maana Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii huwa wanatusaidia sana Elimu ya Afya kuhusu usafi wa mazingira na mambo mengine lukuki” amesema Deus Saule .
MWISHO