Kaimu Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha BoT, Ms Nangi Massawe, Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha maalum kwa watoa huduma za kifedha, iliyofanyika leo Disemba 10, 2024.
Kaimu Meneja wa kumlinda mtumiaji wa Huduma za Fedha, Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, BoT, Dkt. Khadija Kishimba, akifafanua jambo alipokuwa akizungumza katika Warsha hiyo, iliyofanyika katika Ofii za BoT Jijini Dar es Salaam.
Mchambuzi wa Mifumo ya Tehama wa BoT, Laura Mandari ,akitoa mada katika Warsha hiyo namna mfumo huo utakavyofanya kazi.
Meneja Msaidizi Idara ya Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Kifedha, Benki Kuu ya Tnzania BoT, Violet Luhanjo, akizungumza katika warsha hiyo.
PICHA NA; HUGHES DUGILO
DAR ES SALAAM
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kuzindua mfumo wa kidigitali utakaomuwezesha mtumiaji wa huduma za kifedha kuwasilisha malalamiko yake pindi atakapopata changamoto katika Benki anayopata huduma.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha maalum kwa watoa huduma za kifedha, Kaimu Mkurugenzi wa Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha wa BoT, Ms Nangi Massawe amsema kuwa mfumo huo utaanza kufanyakazi mwezi Januari 2025, ili wananchi waanze kuutumia kwa kutuma malalamiko yao.
“Mfumo umetengenezwa na kukamilika, tunaamini ifikapo Januari katikati, tutauzindua rasmi ili wananchi waweze kutuma malalamiko yao, ni muhimu sana kwa kupitia warsha hii tuhakikishe wote tumeuelewa vizuri na kuanza kuutumia kabla ya kuuzindua.” Amesema.
Aidha, Ms Massawe amesisitiza umuhimu wa watoa huduma za kifedha, kuelewa na kuutumia mfumo huo na kuhakikisha unaleta matokeo chanya kwa faida ya Taasisi zao na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande pake Meneja Idara ya Ulinzi wa Watumiaji wa Fedha, BoT, Dkt. Khadija Kishimba, amesema Benki Kuu imeandaa warsha hiyo kwa taasisi za fedha ili kuuelewa mfumo kwani wao ndio wanaokutana na wateja, nakwamba wanapaswa kuueewa kwani mwananchi atatakiwa kuutumia na kutoa malalamiko yake kupitia kiganja chake