Maelfu ya vijana leo wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio la Generation Samia Jogging lililofanyika jijini Dodoma, wakionesha mshikamano wa dhati na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Tukio hilo lililovuta hisia limekuwa nembo ya mshikamano wa kizazi kipya, likidhihirisha jinsi vijana wanavyothamini na kuunga mkono dira ya maendeleo ya serikali.
Wakiwa na ari na nguvu, washiriki walionekana kuwa na furaha na bashasha, huku wakitoa ujumbe wa kumuunga mkono Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.@samia_suluhu_ hassan .
Kwa mujibu wa waandaaji, mafanikio makubwa ya tukio hili yanaashiria azma ya vijana kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kushiriki agenda za maendeleo ya taifa na kumuunga mkono Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, wameahidi matukio zaidi ya aina hii yatakayolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii, kukuza ari ya kizalendo, na kuhamasisha jamii kuishi kwa mtazamo chanya wa maendeleo.