Home LOCAL CHANEL 10 WATAMBUA MCHANGO WA MWAKAGENDA

CHANEL 10 WATAMBUA MCHANGO WA MWAKAGENDA

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda amekishuruku Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten kupitia Kipindi chake cha Masotojo kumpatia tuzo ya heshima kutokana na mchango wake kwenye jamii.
Akizungumzia tuzo hizo Mwakagenda alisema anaishukuru Chanel Ten kwa kumheshimisha kwenye jamii na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa jamii kina anapopata uwezo na nafasi.
“Leo nimepokea tuzo ya heshima kutoka Channel Ten kupitia Kipindi cha Masotojo . Heshima hii ni kubwa sana kwangu na kwa jamii ninayoihudumia, kwani sikujua kuwa matendo yetu yanaonwa na kuthaminiwa na watu wengi.
Kupitia tuzo hii, nimepata motisha ya kuendelea kujitolea na kutumikia jamii yangu kwa bidii zaidi. Ni imani yangu kuwa tuzo hii si yangu pekee bali ni ya kila mmoja aliyeshirikiana nami kufanikisha juhudi zetu za maendeleo na ustawi wa jamii,” alisema.
Alisema anawashukuru waandaaji wa kipindi cha Masotojo kwa kutambua mchango wake, na kwamba jamii imekuwa chanzo cha maono na nguvu za kufanya kazi hizo.
Mwakagenda alisema kwa kufanya kazi pamoja, wanaweza kuleta mabadiliko chanya zaidi. “Naahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uaminifu, na upendo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.
Kwa upande wake muandaaji wa tuzo hizo Mtangazaji wa Chanel Ten, Jacqueline Salon alisema  Mbunge huyo amekuwa na mchango kwenye jamii, hivyo alistahili kupata tuzo hiyo.
“Kipindi cha Masotojo kinahusu mama na baba lishe, lakini pia kinatoa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, tumeweza kufuatilia watu wengi kusema kweli Mbunge Mwakagenda ametugusa, tumeona tumpe tuzo ya heshima ya mwanamke,” alisema.
Salon ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kutoa huduma ambazo zinagusa jamii, ili kusaidia serikali katika kutatua changamoto zilizopo.
Previous articleWAANDISHI WA HABARI MANYARA NA UTPC WAANDAMANA UZINDUZI WA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI
Next articleWEKENI UTARATIBU WA KUSAJILI BIMA MASHAMBA YA MITI- WAZIRI CHANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here