Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!
MLEZI wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa akihutubia maelfu ya wananchi na wanachama wa CCM kwa ujumla katika uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi wa serikali za mitaa katika Mkoa wa Katavi zilizofanyika katika wilaya ya Tanganyika kata ya Ikola uwanja wa like Tanganyijka ‘A’ leo tarehe 20/11/2024.
NA IS-HAKA OMAR, KATAVI.
MLEZI wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amewasihi wananchi wa Mkoa wa Katavi bila kujali tofauti za kisiasa,kidini na kikabila kuweka mbele maslahi ya maendeleo yao kwa kuwachagua kwa kuwapigia kura za ndio wagombea wote wa CCM katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 27 Novemba mwaka 2024 nchini.
Nasaha hizo amezitoa wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika uzinduzi wa kampeni za CCM kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa katika Mkoa wa Katavi,Wilaya ya Tanganyika Kata ya Ikola Kijiji cha Ikola ‘A’ uwanja wa …..
Dkt.Dimwa,alisema kuwa ushindi katika uchaguzi huo una tija na manufaa makubwa kwa wananchi wote sio kwa wanachama wa CCM pekee kwani fursa mbalimbali za maendeleo zitakazopatika kutokana na mipango mzuri ya Viongozi watakaochaguliwa zitawanufaisha wananchi wote.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, alisema wagombea wote wa CCM watakaoshinda kupitia uchaguzi huo watakuwa na kazi ya kuendeleza mikakati ya maendeleo iliyoachwa na Viongozi waliomaliza muda wao wa kiutendaji na uongozi katika miaka mitano iliyopita iliyoleta mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi,kijamii,kisiasa na kimaendeleo hali ambayo ni tofauti kwa vyama vingine vya upinzani vilivyosimamisha wagombea katika mchakato huo.
Pamoja na hayo Dkt.Dimwa, alisema CCM imeendelea kuwa Chama kiongozi katika ubobezi wa kisiasa katika kutekeleza kwa vitendo ahadi zake kupitia utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa manufaa ya wananchi wote mijini na vijiji katika maeneo yote ya Mkoa wa Katavi.
“Wito wangu kwenu wananchi nyote katika Kata zote 58 zilizopo katika Mkoa huu jitokezeni siku ya tarehe 27 Novemba mwaka 2024 mkawapigie kura nyingi wagombea wote wa CCM Ili wakatekeleze nahitaji yenu kwa vitendo.
Pia nawataka wanachama wote wa CCM wekeni tofauti zenu na makundi yenu yote ya wakati wa kura za maoni kwa sasa nyote ni kitu kimoja tunabaki na kundi moja la CCM, kahamasishaneni mkahakikishe Chama cheti kinapata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa”, alisisitiza Mlezi huyo wa CCM Mkoa wa Katavi Dkt.Dimwa.
Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, alifafanua kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza miradi mkubwa kwa dhamira ya kumaliza changamoto za wananchi wa Mkoa wa Katavi ikiwemo mradi wa bandari ya Karema inayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 48.
Aliutaja mradi mingine kuwa ni mradi wa mtandao wa barabara katika Mkoa huo unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 200,mradi wa reli wa kuunganisha reli ya Kaliua,Mpanda hadi Karema pamoja na mradi wa maji kutoka Ziwa Tanganyika kwenda Mpanda Mjini wenye zaidi ya shilingi bilioni 500.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Hassan Kimanta,alisema Chama Cha Mapinduzi kimejipanga vizuri kuhakikisha wagombea wote wa chama hicho wanashinda katika maeneo yao.
“Tunaamini kuwa wananchi wa mkoa wetu wa Katavi bado wana imani na Chama Cha Mapinduzi kutokana na ungwana na utu wa viongozi na watendaji wa Serikali na Chama wanatekeleza kwa vitendo yale waliyoahidi katika kampeni za uchaguzi uliopita.
Hivyo naomba wananchi nyote nendeni mkakibigie kura za ndio wagombea wetu wote ili watuvushe salama katika mikakati ya maendeleo ya sasa na ijayo.”. alisema Idd.
Kupitia mkutano huo wa hadhara Mlezi huyo alitoa nafasi kwa Wabunge na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya za Mkoa huo walieleza kwa ufanisi utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoleta mageuzi ya kimaendeleo katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.
MWISHO