Mkuu wa Mkoa Geita Mhe, Martin Shigella amezitaka Halmashauri za Mbogwe pamoja na Bukombe kuimalisha makusanyo ya Mapatao katika halmashauri hizo.
Alisema hayo Agosti 10, 2022 wakati akiwa kwenye ziara katika wilaya ya Mbogwe na Bukombe akiambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Geita Prof.Godius Kahyarara wamefanya ziara ya kikazi pamoja na kujitambulisha kwa viongozi na watumishi wa Wilaya ya Mbogwe na Bukombe.
Shigella amewataka Viongozi wa wilaya hizo kuweka nguvu ya kutosha katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la mkoa hali itakayo saidia kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Kikubwa kutoka kwenu niombe muwe wabunifu katika kuongeza mapato, wanaokusanya mapato wahakikishe fedha zinapelekwa benki kabla ya kutumiwa mshirikiane, mpendane, mfuuate sheria, taratibu na kanuni za nchi” alisema Shigella.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe, Said Nkumba alikemea tabia chonganishi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambao wamekuwa na tabia ya kusambaza taarifa za uongo kwa viongozi wa kitaifa.