Home BUSINESS WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

WAJASIRIAMALI WA NCHI WANACHAMA EAC WAHAMASISHWA KUWA WABUNIFU

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika tarehe 3 Novemba, 2024 jijini Juba, Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea jijini humo.

Na: Mwandishi Wetu – Juba, Sudan Kusini

WAJASIRIAMALI wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wametakiwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kuongeza ujuzi ili kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Tanzania iliyofanyika tarehe 3 Novemba, 2024 jijini Juba, Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea jijini humo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo, “Kukuza Ubunifu wa Kipekee na Maendeleo ya Ujuzi miongoni mwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki.”

Aidha, Naibu Katibu Mkuu Zuhura Yunus amesema kuwa kauli mbiu ya maonesho hayo inahamasisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutambua na kuthamini suala la kukuza na kuongeza ujuzi na ubunifu kwa wajasiriamali ili kuongeza tija na faida katika utengenezani wa bidhaa zao.

Vile vile, Naibu Katibu Zuhura Yunus ameitaka Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kuyapa kipaumbele maonesho hayo ya ambayo yamekuwa chachu kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kukua kibiashara na kutangaza bidhaa zao.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Annette Mutaawe amesema maonesho hayo yameendelea kuwawezesha wajasiriamali kuongeza uwezo kibiashara na kupanua wigo wa masoko yao kikanda.

Naye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiramali Wadogo na wa Kati EAC (CISO), Josephat Rweyemamu amesema maonesho hayo yamekuwa yakiwavutia Wajasiriamali wengi wa Tanzania kushiriki kwa katika maonesho hayo.

Wajasiriamali walioshiriki katika maonesho hayo wamesema wameweza kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania na wameishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ushiriki wao.

Maonesho hayo ya 24 yamewashirikisha wajasiriamali 1,700 kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakiwemo 299 kutoka Tanzania na yanafanyika kwa mara ya kwanza nchini Sudan Kusini tangu nchi hiyo ijiunge katika jumuiya hiyo mwaka 2016.

Shamrashamra za Wajasiriamali ikiwa ni Siku ya Tanzania ( TANZANIA DAY) katika Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yaliyofanyika Viwanja vya Freedom Hall, jijini Juba, Sudan Kusini.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulrmavu, Zuhura Yunus akizungumza wakati hafla ya Siku ya Tanzania iliyofanyika tarehe 3 Novemba, 2024 jijini Juba, Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea jijini humo.

Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi Mfuko wa NSSF, Bi. Rehema Chuma akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii wakati wa kongamano la wajasiriamali wanaoshiriki katika maonesho hayo ya 24 ya Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika Juba, Sudan Kusini.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa EAC, (CISO Tanzania), Josephat Rweyemamu akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Tanzania (TANZANIA DAY) katika Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika jijini Juba, nchini Sudan Kusini.

Wajasiriamali kutoka Tanzania na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika kongamano kwenye Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi/Jua Kali yanayofanyika jijini Juba, nchini Sudan Kusini.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika viwanja vya Freedom Hall jijini Juba, Sudan Kusini.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus akitembelea mabanda ya wajasiriamali wakati wa hafla ya Siku ya Tanzania (Tanzania Day) katika Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayofanyika jijini Juba nchini Sudan Kusini.

Wajasiriamali wa Tanzania wakionyesha bidhaa mbalimbali wakati wa hafla ya Siku ya Tanzania ( TANZANIA DAY) katika Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yaliyofanyika jijini Juba, Sudan Kusini.

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus akimkabidhi misaada mbalimbali (bidhaa pamoja na fedha) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Fedha na Biashara, Bi. Annette Mutaawe wakati wa Siku ya Tanzania ( TANZANIA DAY) katika Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yaliyofanyika Viwanja vya Freedom Hall, jijini Juba, Sudan Kusini.

Previous articleMTATURU AMPA KONGOLE RAIS SAMIA ASHAURI UWEKEZAJ ZAIDI SEKTA ZA UZALISHAJI
Next articleLISSU AMLIPUA MBOWE ASEMA UPINZANI BADO UNAHITAJI UONGOZI USIO NA MAWENGE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here