Home LOCAL KAMATI YA MWENENDO WACOVID -19 YASHAURI UWEPO WA CHANJO YA UGONJWA HUO.

KAMATI YA MWENENDO WACOVID -19 YASHAURI UWEPO WA CHANJO YA UGONJWA HUO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 17 Mei, 202

DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amepokea Ripoti ya kamati aliyoiunda kuhusu mapendekezo ya Kitalam juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kwamba kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini kikanda na kimataifa. 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud akizungumza mbele ya Mheshimiwa Rais Samia wakati wa kukabidhi Ripoti hiyo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam amesema kuwa kamati yake imetoa mapendekezo kadhaa ya namna ambvyo Serikali inaweza kuyafanyia kazi ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Ameongeza kuwa Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga (interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

Aidha ameongeza kuwa swala la kuwepo kwa chanjo ya COVID –  19 Serikali iendelee na hatua ya kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kutokana na uwepo wa ufanisi na usalama wa kisayansi.

Previous articlePROF. MAKUBI AHIMIZA UFANISI UPIMAJI COVID 19 UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE
Next articleMASHIRIKA YA UMMA YASIYOZINGATIA MWONGOZO WA BAJETI YAFANYIWE TATHIMINI UPYA: DKT. NCHEMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here