Home SPORTS TIMU YA MPIRA WA MIGUU NCAA MABINGWA SHIMMUTA KANDA YA KASKAZINI

TIMU YA MPIRA WA MIGUU NCAA MABINGWA SHIMMUTA KANDA YA KASKAZINI

Timu ya mpira wa miguu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeibuka Bingwa wa Mpira wa miguu katika mashindano yaliyozikutanisha taasisi mbalimbali za Serikali zilizopo mikoa ya Kanda ya kaskazini.

NCAA imeibuka Bingwa katika mchezo wa fainali baada ya kuichapa timu ya K.C.MC kutoka kilimanjaro kwa ushindi wa goli 1-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Chuo kikuu cha Sayansi cha Nelson Mandela Arusha.

Mashindano hayo ambayo ni maandalizi ya michezo ya Shirikisho la Michezo ya mashirika ya Umma, taasisi na Makampuni binafsi (SHIMMUTA) yatakayofanyika kitaifa Jijini Tanga kuanzia tarehe 8 Novemba, 2024 kwa kanda ya Kaskazini yameshirikisha timu za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Chuo cha Nelson Mandela, KCMC, AICC, Chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru, TPHPA, ATC, TAEC na IAA.

Katika hatua Nyingine timu ya mpira wa mikono (Netball) ya NCAA imekuwa mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambapo bingwa wa Netiball ni Chuo kikuu cha Sayansi cha Nelson Mandela.

Previous articleMAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA SI YA TAKUKURU PEKEE-MAJALIWA
Next articleMAJUKWAA YA DINI YATUMIKE KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here