Home LOCAL WAZIRI MKUU AIKABIDHI TAKUKURU MAGARI 88

WAZIRI MKUU AIKABIDHI TAKUKURU MAGARI 88

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa.

Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” Amesema Bw. Crispin

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Previous articleMTIFUANO MKALI, USAHILI BONGO STAR SEARCH AFRIKA KUANZIA ARUSHA 
Next articleWANANCHI ZAIDI YA 15,000 WA KATA YA MAKURO KUPATA MAWASILIANO YA SIMU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here