Home LOCAL BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA...

BARABARA YA LAMI YA KM 7.7 YENYE THAMANI YA BILIONI 9.3 KUUNGANISHA MIKOA YA SINGIDA-SIMIYU-ARUSHA

Wakazi wa Wilaya ya Iramba na Mkalama, Mkoani Singida, wanatarajia kunufaika na barabara ya kiwango cha lami inayojengwa kuunganisha mikoa ya Singida, Simiyu, hadi Arusha. Mradi huu, wenye thamani ya shilingi bilioni tisa, umefikia asilimia 65 ya utekelezaji.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, ametembelea na kukagua mradi huo ambao ukikamilika utawasaidia wananchi katika usafirishaji wa mazao ya kilimo, hivyo kuimarisha biashara.

Amesema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo unaoonesha namna Serikali inavyofanya kazi kubwa ya kutekeleza mradi ya maendeleo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi wake bila ubabaishaji.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoani Singida, Msama Msama, alieleza kuwa kipande cha barabara kinachojengwa kati ya Kitukutu-Gumanga-Mkalama na Chemchem-Sibiti, kikiwemo Kitukutu-Kinampanda, chenye urefu wa kilomita 7.7, kitagharimu bilioni 9.31 na kinajengwa na mkandarasi mzawa.

“RAIS SAMIA NA MAENDELEO, WASIKIE NA WAONE”.

Previous articleMHE.PHILIP MPANGO AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA NISHATI YA JOTOARDHI  KUSHIRIKIANA NA TANZANIA
Next articleTANZANIA YANG’ARA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAJARIBIO WA BIASHARA AFCFTA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here