Home BUSINESS PROGRAMU YA (IMASA) YA  IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA-YAWAFIKIA WANANCHI ZAIDI YA...

PROGRAMU YA (IMASA) YA  IMARISHA UCHUMI NA MAMA SAMIA-YAWAFIKIA WANANCHI ZAIDI YA 90,000.

Katibu Mtendaji wa BARAZA la Taifa la Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa  akizungumza alipokuwa akifungua rasmi kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Octoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa NEEC Neema Mwakatobe, akitoa mrejesho kwenye kikao kazi  kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Kamati Tendaji, Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, Salim Said Salim, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, katika kikao kazi  kilichofanyika leo Octoba 22,2024, katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEF Anitha Mendoza (wapili kushoto) akiwa pamoja na wahariri wengine wakifuatilia mkutano huo.

Dar es salaam.

BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limesema hadi sasa watu elfu tisini (90,000) wamesajiliwa kwenye Kazidata ya programu maalum ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA).yenye lengo la kuinua uchumi wa watanzania yakiwemo makundi maalum.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Baraza hilo kwenye kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika leo Octoba 22, 2024 Jijini Dar es Salaam.

Mwakatobe amesema kuwa programu ya IMASA inatekelezwa kwenye mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na Mikoa Mitano ya Zanzibar, na kwamba kwasasa wapo kwenye hatua ya kwanza ya programu hiyo na tayari wametembelea mikoa 24 ya Tanzania Bara na utekelezaji wake unatarajia kuanza mwaka wa fedha 2024/2025.

Tumejadiliana na viongozi wa mikoa kuhusu shughuli za kiuchumi zinazopatikana kwenye maeneo yao ambazo zitawanufaisha wananchi. Tunaibua vipaumbele ambavyo vitagusa makundi mbalimbali, akinamama, vijana na walemavu, “ amesema Neema.

Ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza, wataingia kwenye awamu ya pili ambayo itahusisha upelekaji wa fursa na programu kulingana na shughuli za kiuchumi walizoziona kwenye mikoa waliyotembelea. “Programu hii ya IMASA inazitambua Programu nyingine zilizopo nchini ikiwemo BBT.”

Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho, Katibu Mtendaji wa NEEC Bi. Beng’i Issa, amesema kuwa Baraza hilo limekuwa likichukua hatua mbalimbali kuwafikia wananchi kote nchini kuwapa elimu ili kufahamu fursa mbalimbali zilizopo za uwezeshwaji kiuchumi na mitaji. 

Aidha amesema kuwa pamoja na maeneo mengine pia wanatoa elimu ya kuimarisha mfumo wa elimu ya ujasiriamali na mazingira ya uwekezaji.  

Previous articleDKT. MWAMBA AJADILI UFADHILI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI
Next articleANATIBU UGONJWA WA KIFUA KIKUU KWA ASILIMIA 100
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here