Home LOCAL MPASUKO MKUBWA ALIOUACHA LISSU IKUNGI: MBINU ZA UPINZANI KUGAWA WATU ZAFICHUKA

MPASUKO MKUBWA ALIOUACHA LISSU IKUNGI: MBINU ZA UPINZANI KUGAWA WATU ZAFICHUKA

Huko Singida, wilaya ya Ikungi, siasa za uadui na chuki zinazoenezwa na Tundu Lissu zimeacha mpasuko mkubwa miongoni mwa wanachama wa Chadema.

Siasa hizi za chuki zinazo anzia ngazi ya taifa, sasa zimefika mpaka kwa wanachama wa ngazi za chini.

Lissu amechochea mgawanyiko kila kona anapopita, na kuacha uhasama mkubwa kutokana na ugomvi wake na Mbowe.

Lissu, ambaye siasa zake zinalenga kulipiza kisasi na kueneza chuki bila kujali maslahi ya Watanzania, amechagua kutumia mgawanyiko kujinufaisha kisiasa.

Huko Ikungi, ameacha machafuko, akiwaacha wana-Chadema katika hali ya kuchanganyikiwa baada ya kuwasha moto wa fitina. Hii ni kawaida kwa upinzani – kueneza chuki na kugawa jamii bila kutoa suluhisho lolote.

Wakati Lissu na wenzake wanazidi kueneza chuki, Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kujenga amani na kuleta maendeleo kwa Watanzania wote. Uongozi wake unalenga kutatua migogoro na kujenga mazungumzo ya kidemokrasia, tofauti kabisa na uharibifu unaosababishwa na siasa za Lissu.

Mbinu hizi za upinzani kuchochea mgawanyiko ni ishara ya wazi kuwa hawako tayari kuongoza jamii pana ya Watanzania. Lengo lao ni kudhoofisha maendeleo ambayo Tanzania imefikia, na Ikungi ni mfano hai wa jinsi siasa zao za chuki na fitina zinavyoweza kuharibu jamii.

Ni wazi kabisa kwamba ajenda ya upinzani sio kujenga bali ni kubomoa. Ni lazima tuungane na viongozi kama Rais Samia ambaye anafanya kazi usiku na mchana kuwaunganisha na kuwawezesha Watanzania wote.

Previous articleWANAWAKE WAHIMIZWA KUCHUKUA MIKOPO INAYOTOLEWA NA SERIKALI KUJIKWAMUA KIUCHUMI
Next articleWAFUGAJI WAMETAKIWA KUACHA KUFUGA KWA MAZOEA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here