Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 14 Oktoba, 2024 amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 149 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (CICG) mjini Geneva, Uswisi.
Mkutano huu unalenga kujadili mada kuu inayohusu “Matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa ajili ya mustakabali wa Amani na Uendelevu.” Mkutano huu umehudhuriwa na takribani washiriki 1,500 wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wakuu wa Misafara pamoja na Wabunge. Mkutano unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 17 Oktoba, 2024 kwa kutoa maazimio muhimu yatakayolenga kutatua changamoto za kimataifa zinazoikabili dunia kwa sasa.