NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mawakala wa ujenzi wa barabara hapa nchini wametakiwa kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha miundombinu ya barabara za wilaya zinazo unganisha mikoa hapa nchini ili kuweza kutatua changamoto kwa haraka na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe wakati wa akifungua wa Semina ya mawakala wa ujenzi wa barabara kutoka katika nchi saba za Africa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ambapo alisema kuwa ni wakati wa Mawakala wa barabara katika mataifa yote kufanya kazi kwa pamoja ilikuondoa changamoto zinazoweza kuepukika.
Mwaisumbe ameeleza kuwa kumekuwa na changomoto kubwa katika ujenzi wa madaraja hasa katika nchi za Africa hasa mvua zinaponyesha kutojana na mafuriko kubeba madaraja na kuacha ugumu kwa wananchi na kuweza kupunguza mapato kwa serikali hasa katika kuchochea ukuaji wa uchumi.
“Mawakala wote wa ujenzi wa barabara mliopo hapa mnatakiwa kuwa wenye uharaka kwa wanachi ili kuboresha maiundombinu kwa jamii hasa katika ujenzi wa madaraja bora yenye kukizi mahitaji ilikuondoa changamoto zinazo epukika kwani bado kuna changamoto za barabara zinazo unganisha barabara kubwa za miji“. Aliwleza Dc Mwaisumbe.
“Kwa wakala wa hapa kwetu Tanroad kwa kushirikiana na Tarura wanatakiwa kuwa na takwimu husika ili kuondoa vikwazo vya barabara kwa wananchi wa vijijini maana huko ndiyo kuna mazao mengi yanayo letwa mijini mnapaswa kuunganisha barabara za wilaya na mikoani tena ziwe barabara zente ubora kwa ukuaaji na ustawi wa uchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla”. Ameeleza Dc Mwaisumbi.
“Katika nchi yetu tunajua serikali imefanya kazi kubwa kwa awamu ya tano na hii awamu ya sita inayo ongozwa na Mh Samia Suluhu Hassan, katika upande wa miundombinu hasa ujenzi wa barabara tumefanya kazi nzuri sana ingawa bado kuna changamoto kadhaa”. Alisema Mwaisumbe.
Kwa upande wake Katibu mtendaji wa TARA, Haghaid Dishanga akieleza kuwa ili kuwa na uchumi madhuti kunategemea sana miundombinu ya barabara kwa wanachi ambao ni wafanya biashara hasa katika nchi za Afrka.
“Kwa mkutano huu mahususi wa wataalamu wa barabara kutoka nchi hizi saba za Africa tunategemea kuwa na mifumo endelevu ya baraba baora kwa malengo ya kuchochea uchumi kwa mataifa yetu ambayo bado tunategemea miundombinu ya barabara kwa kiasi kikubwa”. Alisema Eng Dishanga.
“Ingawa bado kunachangamoto mbalimbali hapa nchini ikiwemo fedha inayotengwa kwa unjenzi na matengenezo ya barabara bado haikidhi mahitaji, kutokujua takwimu za barabara na mifumo yake ikiwa ni pamoja na sera zetu za barabara kwasasa bado hazikidhi mahitaji na zinatakiwa zibadilishwe ili ziwe zenye kukidhi mahitaji “. Alisisitiza.
Aidha alifafanua kuwa lengo kuu la mkutano wa mawakala wa ujenzi wa barabara ni kujua na kupata ufumbuzi wa changamoto za barabara katika nchi za Africa ikiwemo Tanzania ili kuepusha serikali kuingia kwenge gharama kubwa katika ufanyaji wa matengenezo wa barabara.
Alisema ukubwa wa gharama za merekebisho ya barabara yanatokana na kutokujua takwimu za sahihi za barabara zinahitaji nini, tunahitaji kuweka mifumo mizuri ya utambuzi ili kuisaidia serikali kutokufanya marekebisho makubwa ambayo gharama zake ni kubwa