Home BUSINESS WAZIRI MAVUNDE AVUTIWA NA KIJIJI CHA STAMICO MAONESHO YA MADINI GEITA

WAZIRI MAVUNDE AVUTIWA NA KIJIJI CHA STAMICO MAONESHO YA MADINI GEITA

Waziri wa Madini,Mhe.Anthony Mavunde amevutiwa na ubunifu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wa kuwaweka wadau wake eneo moja kwenye Maonesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Mhe.Waziri ametoa pongezi hizo leo tarehe 9 Oktoba wakati alipotembelea banda la STAMICO ambalo limepewa jina la “Kijiji cha STAMICO na Wadau Wake”.

Alivutiwa jinsi washiriki walivyojipanga kwa bidhaa mbalimbali kwenye sekta ya madini.

Pia alivutiwa na vikundi vya wanawake,watu wenye ualbino na watu wenye ulemavu wa usikivu ambao wanashiki kwenye maonesho haya kwa udhamini wa STAMICO.

Mhe.Waziri aliambatana kwenye ziara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhe.Martin Shigela pamoja na maofisa wengine kutoka serikalini.

Vikundi ambavyo vimealikwa na STAMICO na kushiriki ndani ya banda moja ni pamoja na FEMATA,TAWOMA, TAMAVITA,FDH,Tanzania Youth Miners na Chama cha Wachimbaji Geita (GEREMA).

Wengine ni pamoja na kikundi cha Wanawake na Samia Geita na Chama cha Wanawake Geita (GEWOMA

Mhe.Waziri amepokelewa na Kaimu Meneja wa Masoko na Mahusiano wa STAMICO,Bw Gabriel Nderumaki ambae alimpatia maelezo mafupi kuhusu ushiriki wa Shirika kwenye maonesho haya mwaka huu.

Bw Nderumaki amesema kuwa STAMICO inajivunia kufanya kazi na vikundi mbalimbali vya wachimbaji na kuongeza kuwa Shirika litaendelea kuvilea hivi vikundi.

Previous articleMAKAMU WA RAIS AKIWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UKUMBI WA MIKUTANO UYUI
Next articleBoT: WANAWAKE WACHIMBAJI TUMIENI FUSHA ZILIZOPO KWENYE TAASISI ZA FEDHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here