Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Wakazi wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 huku akihamasisha wananchi wote wanawake kwa wanaume wenye sifa kuchukua fomu ili kuwania nafasi za uongozi ngazi ya mtaa, kijiji na kitongoji.
Mhe. Macha ametoa rai hiyo leo Jumanne Oktoba 8,2024 wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga litakaloanza tarehe 11.10. 2024 hadi 20.10.2024 likiongozwa na Kauli mbiu “Serikali za mitaa, sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi”.
“Akina mama wamechangamka sana safari hii, tuhakikishe tunapata uongozi wa pamoja hivyo niwaombe wanaume kwa wanawake tujitokeze kugombea nafasi za uongozi kwa sababu uchaguzi utafanyika ukizingatia makundi yote ya watu katika jamii. Tunawatia moyo watu wote wajitokeze kugombea nafasi za uongozi wanaojua kusoma na kuandika wenye umri kuanzia miaka 21, mwenye akili timamu ,raia wa Tanzania,”,amesema Mhe. Macha.
Amesema uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 katika mkoa wa Shinyanga utafanyika katika Mitaa 90, vitongoji 2704 na vijiji 506.
Aidha Macha amewasihi wananchi wachague viongozi bora na wanaojulikana watakaowaletea maendeleo badala ya kuchagua viongozi mafisadi wa kuhujumu miradi ya maendeleo.
“Tuwachague viongozi bora, tusichague viongozi watakaoleta serikali za matata. Tupate viongozi bora, wasiwe sehemu ya mafisadi wa miradi yetu. Niwapongeze viongozi wa serikali za mnaomaliza muda wenu lakini mnaruhusiwa kugombea tena wananchi ndiyo wataamua”,amesema Macha.
Hata hivyo amesema uchaguzi utakuwa wa huru na haki na serikali imejipanga vizuri kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kuwepo kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
“Tunataka kuwe na amani, wananchi msishawike kutafuta uongozi kwa njia za ugomvi. Hatuendi kugombania uongozi, tunakwenda kugombea, ukisikia mtu anasema anaenda kugombania uongozi ujue anataka kufanya fujo. Tunataka uchaguzi uwe wa haki na amani”,ameongeza Mhe. Macha.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga , Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amewataka wananchi kutumia vizuri muda wa kujiandikisha kila mmoja ajiandikishe kwani suala hilo linafanyika kwa misingi ya haki na amani.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Charles Dominic Kafutila amesema halmashauri hiyo ina kata 17, vijiji 17, vitongoji 84 na mitaa 55 na zoezi la uandikishaji wapiga litafanyika katika vituo 199 ambapo lengo la Halmashauri ni kuandikisha wapiga kura 120,345.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza leo Jumanne Oktoba 8,2024 wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Charles Dominic Kafutila akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga , Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Said Kitinga akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Burudani ikiendelea wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Burudani kutoka Jeshi la Jadi Sungusungu Bugimbagu ikiendelea wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wakiwa na Jeshi la Jadi Sungusungu Bugimbagu wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha na viongozi mbalimbali wakicheza na Jeshi la Jadi Sungusungu Bugimbagu wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro wakicheza na Wanakwaya wa AIC Kambarage wakati wa Uzinduzi wa Zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura Serikali za Mitaa 2024 katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.